Simba wa Ford Kenya anguruma Kabuchai

Simba wa Ford Kenya anguruma Kabuchai

Na CHARLES WASONGA

CHAMA cha Ford Kenya kimehifadhi kiti cha ubunge cha Kabuchai baada ya kuandikisha ushindi mkubwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika Alhamisi.

Kulingana na matokeo rasmi yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Ijumaa asubuhi mgombea wa chama hicho cha Simba Majimbo Kalasinga aliibuka mshindi kwa kuzoa kura 19, 274.

Alifuatwa kwa umbali na mgombeaji wa Chama cha United Democratic Alliance (UDA) Evans Kakai aliyepata kura 6,455.

UDA kinahusishwa na Naibu Rais William Ruto na ndio maana idadi kubwa la wabunge wandani wake walifika katika eneo bunge la Kabuchai kuhudumu kama maajenti wa Bw Kakai.

Kiti hicho kilisailia wazi kufuatia kifo cha James Lusweti mnamo Desemba 4, 2020 baada ya kuugua kwa muda mrefu. Marehemu alikuwa akihudumu muhula wa pili bungeni baada ya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza katika uchaguzi mkuu wa 2013.

You can share this post!

Raila njiapanda Pwani ikijitafutia ‘mkombozi’ mpya

Liverpool kurudiana na RB Leipzig kwenye hatua ya 16-bora...