Simbas kuvaana na Diables Barcelona mchuano wa mwisho Afrika Kusini

Simbas kuvaana na Diables Barcelona mchuano wa mwisho Afrika Kusini

Na GEOFFREY ANENE

TIMU ya taifa ya raga ya wachezaji 15 kila upande ya Kenya maarufu kama Simbas imebadilishiwa mpinzani wa mechi yake ya mwisho ya ziara ya Afrika kuwa Diables Barcelona badala ya Cheetahs.

Diables inatoka mjini Barcelona nchini Uhipania nayo Cheetahs ni ya Afrika Kusini.

Mchuano huo, ambao sakatwa Novemba 25, utakuwa wa nne wa Simbas ya kocha Paul Odera. Utachezewa mjini Bloemfontein.

Simbas ilipoteza dhidi ya Carling Champions 87-15 katika mechi ya kirafiki mnamo Novemba 6 mjini Pretoria na 60-24 dhidi ya mabingwa wa Afrika Namibia na kulemea Brazil 36-30 katika mechi ya nusu-fainali na medali ya shaba ya kipute cha Stellenbosch Challenge mnamo Novemba 14 na Novemba 20, mtawalia.

Hakuna sababu zimetolewa kwa badiliko hilo. Diables ilipoteza 99-15 dhidi ya Cheetahs mjini Bloemfontein mnamo Novemba 17. Cheetahs walipata fursa ya kupepeta Diables baada ya wapinzani wao kubaki wachezaji 14 uwanjani kufuatia Sean Snyman kulishwa kadi nyekundu dakika ya tano.

Simbas inatumia mechi hizo kujipiga msasa kabla ya kurejelea kampeni za kufuzu kushiriki Kombe la Dunia 2023 mnamo Julai 2022 itakapovaana na Uganda katika robo-fainali ya Kombe la Afrika 2022 nchini Ufaransa.

  • Tags

You can share this post!

Afueni Rudisha akitangaza atarejea kutimka baada ya upasuaji

Mkitunyima huduma za serikali, basi msituombe kura –...

T L