Simbas wahitimisha ziara na Wahispania

Simbas wahitimisha ziara na Wahispania

Na GEOFFREY ANENE

KENYA Simbas itakamilisha ziara ya majuma matatu nchini Afrika Kusini dhidi ya Diables Barcelona kutoka Uhispania hii leo.

Vijana wa kocha Paul Odera wamezoa ushindi mmoja na kupoteza mara mbili katika kampeni hizo zao za kujiandaa kwa mechi za kufuzu kushiriki Kombe la Dunia 2023 Ufaransa. Simbas walilimwa 87-15 na Carling Champions katika mechi ya kirafiki Novemba 6 mjini Pretoria na kufungua kipute cha Stellenbosch kwa kupigwa 60-24 na Namibia mnamo Novemba 14.

Walichapa Brazil 36-30 mnamo Novemba 20 katika mechi yao ya mwisho ya Stellenbosch Challenge ya kuamua nani kati yao atanyakua medali ya shaba. Watakutana na Barcelona iliyopoteza 99-15 dhidi ya Cheetahs mnamo Novemba 17. Mzawa wa Fiji, Jone Kubu aliyeibuka mchezaji bora wa Stellenbosch Challenge pia atategemewa na Simbas.

You can share this post!

Wazalendo hoi nchini Ghana

Kinda wa Gor Mchezaji Bora Oktoba

F M