Habari Mseto

Simu mpya ya Huawei Y9 2019 yatua sokoni

October 22nd, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Kampuni ya kutengeneza simu ya Huawei imezindua simu mpya katika soko la Kenya.

Simu hiyo Y9 2019, ina teknolojia mpya ya kuhifadhi betri na aina mpya ya CPU, kamera upande wa nyuma na nyingine upande wa mbele.

Simu hiyo itakuwa ikiuzwa kwa Sh24, 990  katika maduka yote ya kielektroniki na duka la kimtandao la Jumia.

Ukubwa wa simu hiyo inchi 6.5.

“Tunafurahia kutangaza kuwasili kwa Huawei Y9 2019 sokoni. Tunaamini kuwa watu wengi wataipenda sana hasa miongoni mwa vijana kwa sababu ni ya gharama ya chini na pia ina maumbile ya kupendeza,” alisema msimamizi wa Huawei Mashariki ya Afrika Steven Li wakati wa uzinduzi wake Alhamisi.

Ina ukubwa wa kuhifadhi data ya 64GB na uwezo wa betri ni 4000mAh. Simu hiyo itazinduliwa kwa umma Oktoba 27, 2018 Two Rivers na Thika Road Mall.

Lakini wateja wanaweza kuagiza mapema kupitia duka la kimitandao la Jumia.