Siraj apigana kuhakikisha amevalia jezi ya Harambee Stars

Siraj apigana kuhakikisha amevalia jezi ya Harambee Stars

NA ABDULRAHMAN SHERIFF

BEKI wa Bandari FC Mohamed Siraj amesema jana kuwa amepania kuongeza bidii kuhakikisha anaongeza kiwango cha uchezaji wake kwa nia ya kuwavutia wateuzi wa timu ya taifa ya Harambee Stars.

Akizungumza na Taifa Leo kwa njia ya simu, Siraj ambaye ni mmoja wa wachezaji wanaopendwa na mashabiki wa soka wa Pwani anasema ana nia ya kuhakikisha anashikilia namba yake ya beki wa kushoto wa timu hiyo.

“Ninachokihitaji ni kuhakikisha nashikilia namba yangu kwanza kumridhisha kocha wetu Anthony Kimani pamoja na viongozi wa klabu hiyo kwani naamini kama muajiriwa, nastahili kuwaridhisha matajiri zangu ninayoitekeleza uwanjani,” akasema Siraj.

Mchezaji huyo anasema anafurahia jinsi wanasoka wote wa klabu hiyo wanavyopendana na kuwa sawa na familia moja na akaahidi kucheza kwa moyo wake wote.

“Ninaipenda timu yangu ya Bandari na nitaitumikia kwa uwezo wangu wote,” akasema.

Siraj aliwahi kuchukuliwa kwenye kikosi cha Harambee Stars lakini bado hajacheza hivyo ana moto wa kuhakikisha anavaa fulana ya taifa lake na kuisaidia kufanya vizuri kwenye mechi zake za kimataifa.

Mbali na kuichezea klabu yake ya Bandari, Siraj ana nia kubwa ya kucheza katika mojawapo ya klabu zinazotambulikana huko ng’ambo.

“Nataka kuhakikisha nimefanikiwa kutamba kwenye timu ya Stars,” akasema.

Lakini Siraj anasema angelipendelea kucheza mech izote za timu yake ya Bandari ambayo anaamini marea hii itakuwa ikipigania kushinda taji la ligi kuu.

“Nataka tuhakikishe tunaibuka washindi wa ligi kuu,” akasema Siraj.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Tusikubali hisia za kisiasa zivuruge amani

Achani afokea wanaompinga ugavana Kwale

T L