Habari za Kitaifa

Sitatimua mawaziri wangu, asema Ruto kwenye safu ya X Spaces


RAIS William Ruto amepuuzilia mbali wito wa vijana kufanyia mabadiliko baraza zima la mawaziri na kuteua wapya.

Akizungumza katika kikao cha moja kwa moja cha X Spaces, Rais Ruto alifafanua kuwa atazingatia njia nyingine za kushughulikia masuala yaliyoibuliwa na wananchi dhidi ya baadhi ya mawaziri.

Kulingana na Ruto, tayari amepanga hatua kadhaa kushughulikia masuala ambayo yamepaka tope baraza lake la mawaziri.

“Sitalivunja Baraza la Mawaziri kwa sababu niko katika harakati za kuangalia mambo kwa njia tofauti,” Rais Ruto alisema.

Hata hivyo, Rais Ruto aliwaonya mawaziri dhidi ya kujihusisha na shughuli za ufisadi na kusema kuwa yuko tayari kumfuta kazi waziri yeyote.

Miongoni mwa matakwa ya vijana walioandamana ni mawaziri wanaohusishwa na ufisadi wafutwe kazi.