Siwezi kufanya kazi na Raila, Ruto asema

Siwezi kufanya kazi na Raila, Ruto asema

Na SAMMY WAWERU

NAIBU wa Rais William Ruto amepuuzilia mbali uwezekano wake kushirikiana na kiongozi wa ODM Raila Odinga katika mahesabu yake kuingia Ikulu 2022.

Akionekana kumsuta Waziri huyo Mkuu wa zamani, Dkt Ruto amesema sera zake haziwiani na za Bw Raila.

Alisema huku Raila akiendesha kampeni za kutaka Katiba ibadilishwe, chini ya Ripoti ya Mpango wa Maridhiano (BBI) ambayo hatma yake kwa sasa iko mikononi mwa mahakama ya rufaa, Ruto anatetea kuboresha uchumi.

“Tufanye kazi gani na yeye ilhali mambo anayosimamia, sera zake ni tofauti na zetu?” Ruto akahoji, akionekana kumcharura Bw Odinga.

“Anaamini tubadilishe Katiba, kuwe na kiti cha Waziri Mkuu. Sisi sera zetu ni kuinua mwananchi wa kawaida. Hata hivyo, hatuna uadui wala chuki, ila sera zetu ndizo tofauti,” akaelezea.

Dkt Ruto ni kati ya viongozi na wanasiasa waliotangaza azma yao kuwania urais 2022.

Hata ingawa hajaeleza bayana, wandani wa Bw Raila wanadai kiongozi huyu wa ODM atakuwa debeni.

You can share this post!

Nilipokuwa Naibu Rais kazi bora ilifanyika – Ruto

CORONA: Mombasa yapiga marufuku matibabu ya nyumbani