Habari MsetoSiasa

Siwezi kumtetea Obado, Raila asema

October 5th, 2018 1 min read

Na RUTH MBULA

KIONGOZI wa Chama cha ODM Raila Odinga amesema hatamtetea Gavana wa Migori Okoth Obado kuhusiana kesi ya mauji ya mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Rongo Sharon Otieno.

Japo alikiri kwamba amepokea simu nyingi zikimtaka amnusuru gavana huyo, Bw Odinga alishikilia kwamba lazima sheria ichukue mkondo wake wala hawezi kuingilia suala hilo.

Vilevile alisema kwamba maangamizi ya Sharon na kijusi wake yanaweza kufananishwa tu na uchawi na Bw Obado hana jingine ila kujitetea kwa kuwa matukio ya kabla na baada ya kifo hicho yanaashiria kwamba alihusika na mauaji hayo.

Waziri huyo mkuu wa zamani alisisitiza kwamba mauaji hayo yataleta nuksi na laana kulingana na utamaduni wa tangu jadi wa jamii ya Waluo.