Sngura wa siasa wasiojua baridi

Sngura wa siasa wasiojua baridi

Na WANDERI KAMAU

UCHAGUZI Mkuu wa Agosti unaonekana kuwa mtihani kwa wanasiasa ambao wamekuwa ‘wajanja’ kisiasa, ambapo hukwepa kuwa kwenye baridi ya siasa hata ikiwa huwa wanashindwa kutwaa nyadhifa wanazowania.

Wanasiasa hao ni pamoja na Gavana Kiraitu Murungi (Meru), Waziri wa Utalii Najib Balala, Gavana Charity Ngilu (Kitui), Waziri wa Ulinzi Eugene Wamalwa, Waziri wa Mafuta John Munyes, Waziri wa Kilimo Peter Munya, Seneta Sam Ongeri (Kisii), Naibu Waziri wa Uchukuzi Chris Obure na Naibu Waziri wa Masuala ya Kigeni Ababu Namwamba.

Bw Murungi alijitosa rasmi kwenye siasa mnamo 1992, ambapo alichaguliwa kama mbunge wa eneo la Imenti Kusini kupitia chama cha FORD. Tangu wakati huo, Bw Murungi hajawahi kushindwa kwenye uchaguzi wowote, licha ya kutumia vyama tofauti vya kisiasa kuwania nyadhifa mbalimbali.

Mnamo 2013, alichaguliwa Seneta wa Meru kupitia APK na kushinda ugavana 2017 kupitia Chama cha Jubilee (JP). Kabla ya hapo, alihudumu kama Waziri wa Haki na Masuala ya Kikatiba katika serikali ya Rais Mstaafu Mwai Kibaki.

Kwa sasa, Bw Murungi amebuni chama kipya cha Devolution Empowerment Party (DEP), anacholenga kutumia kutetea nafasi yake ya ugavana.

Naye Bw Balala amefanikiwa kuwa kwenye siasa au serikalini tangu 2002, bila kujali ikiwa amechaguliwa au la.

Tangu wakati huo, amehudumu kama waziri wa Jinsia, Michezo na Utamaduni, Leba, Turathi za Kitaifa, Madini na Utalii. Kati ya 2002 na 2013 alihudumu katika wizara mbalimbali akiwa mshirika wa Rais Mstaafu Mwai Kibaki na kiongozi wa ODM Raila Odinga.

Mnamo 2013, aliwania useneta katika Kaunti ya Mombasa kupitia chama chake cha Republican Council (RC) lakini akashindwa na Hassan Omar (Wiper). Baada ya kushindwa aliteuliwa na Rais Uhuru Kenyatta kuwa Waziri wa Madini.

Mwaka wa 2017 hakuwania nafasi yoyote ya kisiasa. Hata hivyo, alikuwa miongoni mwa mawaziri waliohifadhi nyadhifa zao baada ya Rais kufanya mageuzi katiika baraza hilo. Amekuwa akihudumu kama waziri wa Utalii tangu Juni 2015.

Bi Ngilu amekuwa kwenye ulingo wa siasa tangu 1992 alipochaguliwa mbunge waKitui ya Kati kwa tiketi ya chama cha DP. Tangu wakati huo, amekuwa akishinda katika chaguzi zote ambazo amekuwa akiwania bila kujali vyama anavyotumia. Baadhi ya vyama alivyotumia kuwania ni DP, SDP na Narc.

Baada ya kushindwa kwenye kinyag’anyiro cha useneta katika Kaunti ya Kitui na Bw David Musila mwaka 2013, aliteuliwa Waziri wa Ardhi na Rais Kenyatta.

Prof Ongeri kwa upande wake amefanikiwa kuwa kwenye ulingo wa siasa tangu 1988, alipochaguliwa mbunge wa Nyaribari Masaba. Alihudumu kama waziri katika wizara za Elimu na Mashauri ya Kigeni katika serikali ya Bw Kibaki.

Hata hivyo, baada ya kushindwa kwenye kinyang’anyiro cha useneta mnamo 2013, aliteuliwa na Rais Kenyatta kuwa Mwakilishi Maalum wa Kenya katika Umoja wa Mataifa (UN).

Kwenye uchaguzi wa Agosti, ametangaza atawania ugavana katika Kaunti ya Kisii.

Bw Wamalwa alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Mbunge wa Saboti mnamo 2003 baada ya kifo cha nduguye, Michael Kijana Wamalwa, aliyekuwa Makamu wa Rais katika serikali ya Kibaki.

  • Tags

You can share this post!

UJAUZITO NA UZAZI: Kiungulia kwa mama mjamzito na njia za...

OKA hatarini kusambaratika vinara wakimenyania tiketi ya...

T L