Makala

Soko la Uhuru linavyowapa riziki wafanyabiashara Nairobi

November 14th, 2020 2 min read

NA KEVIN ROTICH

Kwa zaidi ya miongo minne, Bwana John Saisi amenadhifisha tajriba ya kuunda mpira za kandanda katika soko la Uhuru katika kaunti ya Nairobi.

Kupitia mikono yake mahiri, Bwana Saisi ametunza tajriba nyingi kwenye za shule, mitaa na vilabu k vya kandanda katika maeneo ya Eastland’s.

“Siku ya kwanza nilipokuja kwenye soko hili mwaka wa 1978, nilianza kuuza bidhaa za kawaida kabla ya kuanza rasmi kuunda mipira,” Bwana Saisi anasema huku akiongeza kuw a alijitwika kwenye Nyanja hio kutoka na kupanda kwa umaarufu wake.

Anasema wateja wake ni wamiliki wa shule, watu wa binafsi, supermarkets, baadhi yam engine.

Kutokana na biashara hiyo, amesomesha watoto wake kumi ambao walihitimu hadi vyuo vikuu. Biashara yake imewaajiri zaidi ya watu 20 na wengine wengi.

“Bei ya mipira uanza kutoka Sh1, 00 hadi Sh300, kulingana na umri. Mpira za watu wazima ugharimu Sh1, 000 ilhali ya watoto wa chekechea Sh300,” Bwana Saisi ambaye ana umri wa sabini anasema.

Kwa wastani, yeye huuza mpira kati ya 400 hadi 400 kwa mwezi, ambaye huumpa zaidi ya Sh100, 000.

Yeye uagiza mali ghafi jutika kwa watu wa Juakali na wachuuzi wengineo. Baadhi ya mali ghafi ambayo yeye utumia ni kama vile cowhide, special stitches, glues, rubber bladders and stitchings.

Kwa miaka kadha, wachuuzi wameongeza hadi kufikia 6, 000 kwenye 324 stalls.

Anaomba kaunti ya Nairobi wakarabati mabomba ya maji taka, mwangaza, sehemu ya maegesho la magari na pia ukuta.

“Kama mwekahazina wa soko hili kwa zaidi ya miaka 20, niliiandiakia barua kadhaa uongozi wa kitambo wajenge soko hilo. Lakini, baadhi ya matakwa yao yalishughulikiwa,” anasema.

“Siku za hivi punde, waliweka mabati kwa sababu iliyokuwa hapo mbeleni ilikuwa inaingiza maji na kusababisha uharibifu mkubwa,” anasema.

Anasema kufungwa kwa shule kuliharibu biashara yake kwa sababu alikuwa anawategemea.

Mwezi wa Juni, kaunti ya Naironi ilitangaza kuwa inapanga kufungua soko tano katika maeneo kadha katika kaunti ya Nairobi yatakayotumiwa na zaidi ya wachuuzi 7, 000 mwakani.

Kwa sasa, kaunti ya Nairobi in soko 20 za wazi na 23 kubwa ambazo haziwezi kutumiwa na idadi kubwa ya watu jijini.

Masoko yatakayo imarishwa ni kama Westlands Market, Karandini Market, New Wakulima Market Barbara ya Kangundo , Qware Road Market and Mwariro Market.

Mwezi wa Juni, mkurugenzi wq biashara kaunti ya Nairobi,Fredrick Ndunyu alisema soko hizi zimekamilishwa kwa asilimia tisini na tisa zitakazo kuwa na vifaa vya kisasa vya reja reja na jumla.

Mita chache ni Bwana Stephen Mbugua ambaye amekuwa mchuuzi katika soko hilo kwa miaka 25 iliyopita.

Bwana Mbugua huuza nguo za wanadada. “Apo mbeleni, nilikuwa nikiuza vyombo na mboga kwani chakula ilikuwa ikiuzwa mle.”

Anasema biashara hiyo imemwezesha kuwasomesha wanawe.

“Natengeneza Sh20, 000 kwa wastani,” Bwana Mbugua aliye na umri 64 anasema. Mojawapo ya shida ambazo anapitia ni bidhaa za bei nafuu zinazouzwa katika eneo la Eastleigh.

“Kwa mfano, gharama kubwa ya umeme inakula pesa ambayo ningeweza kupata,”anasema. Mchuuzi mwingine ni Wangeshi Waithaka ambaye anauza nguo za kitamaduni katika soko hilo.

“Ninauza bidhaa zangu katika soko la Maasai Market kwa watalii lakini idadi ya ilipopungua uuzaji ulishuka maradufu.

Ameweza kusomesha wanawe wawili hadi vyuo vikuu na sekondari. Bei ya bidhaa zake huanzia Sh700 hadi Sh3, 000. Kwa bei ya jumla, yeye huuza Sh500.

“Huwa Napata Sh30, 000 kwa mwezi lakini kwa sasa Napata tu Sh5, 000 kutoka na corona,” anasema Hulipia Kodi ya kaunti kutoka Sh2, 000 hadi Sh4, 000, kulingana na kiwango cha duka.