SOKOMOKO WIKI HII: Wajackoyah na mdogowe walivyopigwa na ‘radi’ kali

SOKOMOKO WIKI HII: Wajackoyah na mdogowe walivyopigwa na ‘radi’ kali

NA CHARLES WASONGA

NUSRA mgombeaji wa urais wa chama cha Roots, Prof George Luchiri Wajackoyah ampoteze mwaniaji mwenza wake, Justina Wamae wiki hii kufuatia madai kuwa wakili huyo anamuunga mmoja wa wapinzani wake, Bw Raila Odinga.

Jumatano, Bi Wamae alitisha kuunga mkono mrengo wa Kenya Kwanza “ikiwa itatokea haja ya mimi kuunga mkono mgombea urais mwingine”.

Hii ni baada ya video moja kuchipuka mitandaoni ambako Prof Wajackoyah anasikika, na kuonekana, akimpigia debe Bw Odinga, ambaye ni mgombea urais wa Azimio la Umoja-One Kenya.

Mwanasiasa huyo, ambaye ni wakili, alikuwa ndani ya kilabu kimoja cha burudani jijini Kisumu ambako alikumbana na idadi kubwa ya mashabiki wa “injili” yake kupigania kuhalalishwa kwa bangi na ufugaji wa nyoka.

Saa chache baadaye, Bi Wamae alichemka kwa hasira akisema wanachama wa chama cha Roots hawajaafikiana kuhusu suala la kumuunga Bw Odinga.

Lakini mwanasiasa huyo, ambaye amejaaliwa uwezo wa matumizi ya lugha kwa ufasaha, aliungama kuwa mkubwa wake anashabikia Azimio.

“Ni kweli mkubwa wangu aliye kiongozi wa chama chetu anaunga Azimio. Sisi kama chama cha Roots hatujajadili suala hilo na binafsi kama mgombea mwenza sijajulishwa kulihusu.

“Hebu niseme hivi, endapo nitahitajika kumuunga mgombeaji urais mwingine, basi nitaunga mrengo hasimu,” Bi Wamae aliye na shahada ya uzamili katika Ujasirimali kutoka Chuo Kikuu cha Kikatoliki, alisema katika runinga ya NTV.

Mpasuko ndani ya chama cha Roots unanunikia huku zikisalia saa chache saa chache kabla ya Wakenya kuelekea debeni kuwachagua viongozi wapya.

Hali hiyo pia imejiri wakati baada ya uvumi kuenea kuwa Profesa Wajackoyah ni “mradi” wa serikali anayedhaminiw kwa ajili ya kuharibu kura za mgombea urais wa Kenya Kwanza Dkt William Ruto.

  • Tags

You can share this post!

MALEZI KIDIJITALI: Daima kinga yashinda tiba!

Mkuki kwa Raila, kwa Ruto mchungu

T L