Michezo

Solskjaer asisitiza Pogba hatauzwa

August 7th, 2019 1 min read

Na MASHIRIKA

KOCHA Ole Gunnar Solskjaer wa Manchester United amesema hawatamuachilia kiungo Paul Pogba kuondoka katika klabu hiyo kwa sasa.

Kumekuwa na hofu miongoni mwa mashabiki wa klabu hiyo ya ligi kuu ya Uingereza (EPL) hasa baada ya staa huyo kukosekana kwa kikosi wakicheza na SC Milan, hata baada ya kocha huyo kudai kwamba Mfaransa huyo alikuwa mgonjwa.

Katika mechi hiyo, vijana wa Solskjaer waliibuka na ushindi wa 5-4 kupitia kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya 2-2 katika muda wa kawaida.

Akizungumza na waandishi baada ya mechi hiyo kumalizika, kocha alisisitiza hatauzwa.