Sonko azimwa kurusha video za Kananu

Sonko azimwa kurusha video za Kananu

Na RICHARD MUNGUTI

ALIYEKUWA Gavana wa Nairobi Mike Sonko Mbuvi Ijumaa alizimwa na mahakama kupeperusha katika mitandao ya kijamii video au habari za kushusha hadhi ya Gavana Anne Kananu Mwenda aliyeteuliwa wiki mbili zilizopita..

Akimpiga breki Bw Mbuvi kueneneza katika mitandao habari zozote kuhusu Bi Kanan, hakimu mkuu mahakama ya Milimani Bw Heston Nyaga alisema haki za gavana huyu mpya zapasa kulindwa kabla ya kusikizwa na kuamuliwa kwa kesi aliyomshtaki Bw Sonko.

Akiwasilisha kesi dhidi ya Sonko na Bi Thura Nkatha, Gavana huyu mpya alisema ameahiribiwa sifa na jina kupitia video zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii kumuhusu. Aliomba Bw Nyaga atoe maagizo ya kumzima Sonko na Nkatha wakisambaza video zinazohujumu haki zake.

“Sifa za Kananu zimeshushwa kupitia video na maandishi katika mitandao ya kijamii.Naomba washtakiwa wazuiliwe kupeperusha video nyingine,” hakimu aliombwa na Bi Kananu. Akitoa uamuzi Bw Nyaga alisema mlalamishi amethibitisha kuna uwezekano wa kusambazwa kwa video au habari nyingine zinazoweza kumharibia sifa zake kama Gavana mpya wa Nairobi.

“Baada ya kusikiza ushahidi kutoka kwa mlalamishi nimeridhika kwamba yuko na ushahidi wa kutosha kuthibitisha ameharibiwa sifa kupitia kwa video na mitandao ya kijamii,” alisema Bw Nyaga. Hakimu huyo aliongeza, “Baada ya kuzingatia ushahidi uliowasilishwa Sonko na Nkatha wamezuiliwa kuchapisha ama kupeperusha katika mitandao ya kijamii habari zozote za kumkejeli na kushusha hadhi ya Gavana Kananu.”

Hakimu huyo aliwaamuru washtakiwa wasichapishe katika magazeti au kutangaza katika mitandao ya kijamii habari zozote za kumvunjia heshima Bi Kananu. Bi Kananu aliwasilisha kesi hiyo kupinga hatua ya washtakiwa kuhusika na usabambazaji wa habari kumhusu katika mitandao ya kijamii.

Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani baada ya kipindi cha siku chache cha kusambaza habari za Gavana huyu mpya alizosema zimemharibia. Tume ya huduma za mahakama JSC imemwagiz Sonko afike mbele yake kuhusu masuala hayo

You can share this post!

Diamond League 2022 kuanza Mei 13

Mahakama yakataa kuzima utoaji wa chanjo ya Covid-19 ya...

T L