Habari Mseto

Sonko kujibu mashtaka mapya Voi

December 17th, 2019 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

GAVANA wa Nairobi Mike Sonko, ambaye ameshtakiwa kwa ufujaji wa Sh381 milioni za umma, Jumatano anatarajiwa kufika katika Mahakama ya Voi kujibu mashtaka ya kukataa kutiwa nguvuni na kujeruhi afisa wa polisi.

Bw Sonko aliagizwa na afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) ajisalamishe katika mahakama ya Voi kujibu mashtaka hayo mapya.

Mahakama ya Voi ilitoa kibali cha kumtaka Bw Sonko afike kortini kujibu mashtaka hayo.

“Sonko ataandamana na mawakili wake hadi Voi kujibu mashtaka aliyofunguliwa na DPP,” wakili wake Cecil Miller aliambia Taifa Leo.

Sonko alikamatwa Desemba 6 na maafisa wa polisi kisha akasafirishwa kwa ndege hadi Nairobi na kushtakiwa pamoja na washukiwa wengine 24.

Gavana Sonko alizuiwa na mahakama kuendelea kutekeleza majukumu yake hadi kesi hiyo itakaposikizwa na kuamuliwa.Hali hiyo imeacha Nairobi kweenye utata kwani hakuna naibu gavana.