Makala

Sosholaiti Tanasha akumbwa na ngori ya utapeli wa Sh600, 000

Na SINDA MATIKO June 25th, 2024 1 min read

MWANASOSHOLAITI na mwanamuziki Tanasha Donna ameshtakiwa na mwanamuziki ibuka kutoka Amerika Britanny Jones anayedai mrembo huyo alimtapeli.

Kulingana na kesi hiyo, Jones anaiomba mahakama imshurutishe Tanasha ambaye ni mpenzi wa zamani wa nyota wa bongo flava Diamond Platnumz kumlipa zaidi ya Sh619, 000.
Britanny anayeishi Amerika ameiambia mahakama kwamba aliingia kwenye mkataba na Tanasha ya wao kufanya kolabo na mrembo, ambapo aligharamia mahesabu yote yaliyohitajika ikiwemo kulipa kiasi cha fedha alichoitisha sosholaiti huyo kwa ajili ya kolabo.

Hata hivyo, Jones anasema ni zaidi ya miaka mitatu toka wasaini mkataba huo kwani Tanasha amekuwa akimpiga chenga na amegoma kushiriki kwenye kolabo hiyo.

Sasa anaitaka mahakama kumshurutisha Tanasha kumfidia fedha zote alizotumia kusafiri kutoka Amerika hadi Nairobi kwa ajili ya shughuli ya kuandaa wimbo huo, ila mrembo huyo akawa hapatikani.