SPANISH CUP: Barcelona wapewa limbukeni Cornella waliowadengua Atletico Madrid katika hatua ya 32-bora

SPANISH CUP: Barcelona wapewa limbukeni Cornella waliowadengua Atletico Madrid katika hatua ya 32-bora

Na MASHIRIKA

KIKOSI cha Cornella kinachoshiriki Ligi ya Daraja la Tatu nchini Uhispania, sasa kitakutana na Barcelona katika raundi ya 16-bora ya kipute cha kuwania taji la Spanish Cup msimu huu.

Licha ya ulimbukeni wao, Cornella walipiga Atletico Madrid 1-0 mnamo Januari 6 ugani Wanda Metropolitano na kuwabandua wanasoka hao wa kocha Diego Simeone kwenye mashindano hayo.

Bao la pekee na la ushindi katika mechi hiyo lilifumwa wavuni na Adrian Jimenez.

Barcelona pamoja na Real Madrid, Athletic Bilbao na Real Sociedad ndivyo vikosi vingine vya Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) ambavyo tayari vimefuzu kwa hatua ya 16-bora ya mapambano hayo ya Spanish Super Cup.

Chini ya kocha Zinedine Zidane, Real Madrid wamepangwa kukutana na kikosi kingine cha Ligi Kuu ya Daraja la Tatu (Segunda B), Alcoyano, waliowadengua Huesca katika hatua ya 32-bora ya Spanish Cup kwa mabao 2-1 mnamo Januari 7, 2021.

Bilbao watavaana pia na kikosi kingine cha Ligi ya Segunda B, Ibiza kilichowabandua Celta Vigo kwa mabao 5-2. Real Sociedad watakuwa wageni wa Cordoba.

Mechi zote za hatua ya 16-bora zitasakatwa kati ya Januari 16-21, 2021.

DROO YA HATUA YA 16-BORA YA SPANISH SUPER CUP:

Cornella na Barcelona, Ibiza na Athletic Bilbao, Alcoyano na Real Madrid, Cordoba na Real Sociedad, Pena Deportiva na Valladolid, Navalcarnero na Eibar, Malaga na Granada, Almeria na Alaves, Leganes na Sevilla, Alcorcon na Valencia, Girona na Cadiz, Sporting na Real Betis, Espanyol na Osasuna, Fuenlabrada na Levante, Rayo Vallecano na Elche, Tenerife na Villarreal.

You can share this post!

Maafisa walaumiwa kwa kupendelea watu wa Trump

Oliech kuandaa mechi kubwa ya kuwapa mashabiki fursa ya...