Staa Lewandowski bado yupo Bayern Munich hadi 2023

Staa Lewandowski bado yupo Bayern Munich hadi 2023

IMETAYARISHWA NA CECIL ODONGO

AFISA Mkuu Mtendaji wa Bayern Munich Oliver Kahn, amesema kuwa klabu hiyo inatarajia kuwa nyota wao Robert Lewandowski atawachezea msimu ujao wala haendi popote.

Lewandowski,33, ana mkataba na mibabe hao wa Bundesliga ila kumekuwa na madai kuwa yupo karibu kutua Uhisapania kusakatia Barcelona.

Shinikizo hizo zimezidi baada ya Sadio Mane kujiunga na Bayern kutoka Liverpool na kutambulishwa kwa sherehe ya haiba mnamo Jumatano.

“Lewandowski ana kandarasi nasi hadi 2023 na tunatarajia kumwona mazoezi siku ya kwanza ya mazoezi ya kujifua kabla ya msimu mpya kuanza. Hakuna kilichobadilika. Robert ana kandarasi nasi ambao umesalia mwaka moja utamatike,” akasema Khan wakati wa kutambulishwa rasmi kwa Mane.

Uongozi wa Bayern unashikilia kuwa Lewandowski haendi popote licha ya mchezaji huyo kuwataka kuwa waanzishe mazungumzo na Barcelona ili ahamie Camp Nou.

Nyota huyo raia wa Poland amesakatia Bayern kwa muda wa miaka minane iliyopita tangu ajiunge nao kutoka mahasimu wao Borrusia Dortmund.

Kwa misimu saba ambayo amekuwa na Bayern, Lewandowski amefunga mabao 344 katika mechi 374 alizowajibishwa.

Aliyafunga mabao 238 kwenye Bundesliga na 69 katika Uefa.

  • Tags

You can share this post!

STAA WA SPOTI: Rayton ‘Boom Boom’ Okwiri atamba...

KINYANG’ANYIRO 2022: Kaunti ya Kakamega

T L