Michezo

Starlets kutoana jasho na She-polopolo ya Zambia

March 11th, 2018 1 min read

Na GEOFFREY ANENE

TIMU ya taifa ya soka ya wanawake ya Kenya itajipima nguvu dhidi ya Zambia hapo Machi 25, 2018.

Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) limetangaza Ijumaa kwamba Harambee Starlets itakabiliana na She-polopolo uwanjani Arthur Davies mjini Kitwe. Itatumia mchuano huu kujipiga msasa kabla ya kumenyana na Uganda katika mechi ya kufuzu kushiriki Kombe la Afrika mwaka 2019.

“Tunaamini mechi ya kirafiki dhidi ya Zambia itatupa fursa tunayohitaji ya kujipima nguvu kabla ya kukutana na Uganda,” Kocha Mkuu wa Harambee Starlets, Richard Kanyi amesema.

Starlets tayari imeanza mazoezi katika uwanja wa Kenyatta mjini Machakos. Itaanzia kampeni yake ya kufuzu nyumbani hapo Aprili 4 kabla ya kuelekea nchini Uganda kwa mechi ya marudiano siku tatu baadaye.

Kombe la Afrika litafanyika Novemba 17 hadi Desemba 1 mwaka 2018 nchini Ghana.