Stephen Mule ahifadhi kiti cha eneobunge la Matungulu

Stephen Mule ahifadhi kiti cha eneobunge la Matungulu

NA WYCLIFFE OTIENO

KATIKA eneo la Matungulu shughuli ziliisha vyema.

Mheshimiwa Stephen Mule wa Wiper alihifadhi kiti chake baada ya kuzoa kura 17,703.

Mpinzani wake wa karibu Dkt Philip Munyao alizua taharuki alipolalamika kuwa Bw Mule alishirikiana na maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kumwibia kura. Hata hivyo aliondoka kwa haraka akisema yote ameachia Mungu. Dkt Philip alipata kura 13,878.

Matokeo ya Urais katika Eneobunge la Matungulu

Raila Odinga – 33,270

Dkt William Ruto – 11,991

David Mwaure – 146

Profesa George Wajackoyah – 344

Idadi ya Wapigakura Waliosajiliwa ni 76,088

Kura halali – 45,751

Kura zilizoharibika – 399

  • Tags

You can share this post!

Ruto na Raila wafuatana unyounyo kwenye matokeo ya urais

GWIJI WA WIKI: Nancy Okware

T L