‘Straika’ Mbrazil aliyeshindwa kupepetea K’ Ogalo

‘Straika’ Mbrazil aliyeshindwa kupepetea K’ Ogalo

Na  JOHN ASHIHUNDU

MASHABIKI wa Gor Mahia watazidi kukumbuka mnamo 2013 wakati klabu yao ilitaka kuweka historia, kwa kuwa timu ya kwanza nchini kusajili mwanasoka kutoka Brazil.

Lakini baadaye barobaro huyo aligeuka na kuwa mtalii aliyekuja nchini kwa shughuli tofauti.Baada ya sifa tele kupitia kwa vyombo vya habari, Gor ilimleta nchini Giovanni Rodriquez.Mashabiki waliomiminika uga wa City Stadium kumshuhudia mazoezini waliondoka wakiwa na mshangao mkubwa, baada ya mshambuliaji huyo kushindwa kupepeta mpira.

Mashabiki wa K’Ogalo walimtarajia angebadilisha sura ya Ligi Kuu ya Kenya (KPL), kumbe walihadaiwa na ajenti mmoja maarufu aliyedai alikuwa na DVD za nguvu za mchezaji huyo.Wakati wa mazoezi ugani City, Rodriquez, ambaye alizaliwa 1998, alianguka mtihani.

Miongoni mwa mashabiki hao uwanjani walikuwemo wafuasi wa mahasimu wa jadi AFC Leopards, waliofika hapo kujaribu kumpokonya Mbrazil huyo akubali kuchezea timu yao ya Ingwe.Mara tu alipopewa mpira aonyeshe mbinu zake kali hadharani, kocha Zdravko Logarusic alipigwa na butwaa mbele ya kamera, pamoja na waandishi wa habari waliofika uwanjani humo kudondosha taarifa za Rodriquez.

Hatimaye aliamua kwenda likizoni Pwani kabla kuondoka nchini siku chache baadaye kurejea kwao.’Baada ya kumfuatilia kwa wiki moja, sioni akifaulu kuelewa mfumo wangu. Ni mzito zaidi na anahitaji mazoezi magumu ili apunguze uzito.

Ni mtu aliye na matatizo mengi ya binafsi na sidhani atatusaidia,’ hayo yalikuwa maoni ya kocha Logarusic, wakati huo akisaidiana na John Bobby Ogolla.’Nimeanza kufikiria huyu sio mchezaji tuliotazama kwenye video. Na ni yeye pasi ilikuwa video ya zamani sana,’ aliongeza katibu wa Gor Mahia wakati huo, Ronald Ngala.

Gor Mahia walikuwa tayari wameandaa mkataba wa miaka miwili ambapo Rodriguez alitarajiwa kulipwa Sh150,000 kwa mwezI.

You can share this post!

Mmiliki wa Hoteli kukamatwa kwa ulaghai wa Sh.520Milioni

‘Bobby’ Ogolla yule kipenzi cha mashabiki

T L