Michezo

Straika wa Nzoia atwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Aprili

May 29th, 2018 1 min read

Na CHRIS ADUNGO

STRAITA matata anayeongoza kwa usogora wa kufuma magoli kwene Ligi Kuu ya Kenya msimu huu, Elvis Rupia amejizolea tuzo ya Mchezaji Bora wa Aprili.

Rupia, ambaye amefunga jumla ya mabao 12 katika mechi 16, aliwabwaga washindani wawili wa Zoo Kericho Michael Madoya na Nicholas Kipkurui na kutwaa tuzo hiyo.

Mshambuliaji huyo wa Nzoia Sugar alipiga mabao manne mwezi Aprili sawa na wawili hao, lakini akachaguliwa kwa tuzo hiyo.

Ubora wa mbinu zake ulimpa pointi mbili zaidi ya Kipkurui ambaye aliibuka namabri mbili akiwa na pointi 17. Madoya, mchazaji mwenye thamani ya juu zaidi ligini, aliibuka wa tatu kwa pointi 15.