Kimataifa

Sudan na Ethiopia zashirikiana kulinda mpaka

September 3rd, 2018 1 min read

MASHIRIKA Na PETER MBURU

JUBA

Mataifa ya Ethiopia na Sudan Kusini yameingia katika mkataba wa kuunda kikosi kimoja cha kulinda mpaka baina yao, ili kukomesha usafirishaji wa silaha baina ya mataifa hayo.

Baada ya kikao cha siku mbili baina ya walinda usalama wa mataifa hayo mawili, mkataba huo ulitiwa saini Jumatano wiki iliyopita.

Akiwakilisha Sudan Kusini, Gavana wa jimbo la Boma Gen David Yau Yau na Dkt Gatluak Tut Khot, rais wa eneo la Gambella Ethiopia walitia saini mkataba huo, wakianzisha rasmi kikosi cha ulinzi cha pamoja.

“Kunafaa kuwa na kikosi kimoja cha ulinzi wa mpaka huu ili kuvurugua vikundi vinavyoharibu amani na biashara haramu zinazoendeshwa mipakani,” mkataba ukasema.

Mataifa hayo mawili aidha yameeleweana kushirikiana zaidi kuinua elimu na biashara.

Walijutia kuwa mavamizi ya mipakani yaliyotekelezwa eneo la Gambella na kikosi kutoka Sudan Kusini 2016 yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 200 na zaidi ya watoto100 kutekwa nyara yangesuluhishwa.

Watoto 50 walirejeshwa lakini wengine hawajawahi kuonekana tena. Katika makubaliano hayo, Ethiopia iliitaka Sudan Kusini kurejesha watoto hao.