Kimataifa

Sunak asitisha mpango wa kusafirisha wakimbizi kutoka Uingereza hadi Rwanda

May 24th, 2024 1 min read

LONDON, Uingereza

MPANGO tata wa kusafirisha maelezo ya wakimbizi kutoka Uingereza hadi Rwanda huenda usitekelezwe baada ya Waziri Mkuu Rishi Sunak kuzima shughuli hizo kabla ya uchaguzi wa kitaifa utakaofanyika Julai mwaka huu.

Baada ya kuingia afisini mnamo Oktoba 2022, Sunak alianzisha mpango wa kusafirisha watu hao waliingia Uingereza bila idhini na kuwapeleka Rwanda.

Alitaja hatua hiyo kama moja ya sera zake kuu akielezea matumaini kuwa itazuia maelfu ya wakimbizi kuingia nchini humo haswa kwa kutumia mashua.

Mnamo Aprili mwaka huu Sunak aliahidi kuwa ndege ya kwanza iliyobeba watu hao ingeondoa baada ya wiki 10. Hi ni baada ya bunge la Uingereza kupitisha mswada ambao ulioondoa vikwazo vya kisheria vilivyozuia utekelezaji wa mpango huo kwa zaidi ya miaka miwili.