Habari Mseto

Supamaketi ya mwandani wa Ruto yavamiwa Emali

Na PIUS MAUNDU July 4th, 2024 1 min read

KUNDI la vijana waandamanaji limevamia duka la supamaketi linalohusishwa na mfanyabiashara James Mbaluka, mwandani wa karibu wa Rais William Ruto, mjini Emali.

Tukio hilo la Alhamisi, Julai 4, 2024, adhuhuri lilijiri wakati mamia ya vijana waliokuwa wamekusanyika kuanza maandamano ambayo hayakufanyika katika miji mingi kama ilivyokuwa inatarajiwa, walipofululiza hadi kwa supamaketi hiyo iliyoko kando kando mwa barabara kuu ya Mombasa-Nairobi.

Waliiba mali ya thamani isiyojulikana huku maafisa wa ulinzi wakilemewa na idadi kubwa ya waporaji hao.