Makala

SWAGG: Jamie Foxx

April 16th, 2019 2 min read

JINA lake la kuzaliwa ni Eric Marlon Bishop, jina ambalo ukiwatamkia mamilioni ya mashabiki wake, utawachanganya sana mpaka pale utamwita Jamie Foxx.

Foxx ni mdau mkubwa wa burudani akiwa amejaliwa vipaji chungu nzima vinavyomfanya kuwa katika levo ya juu sana kwenye ulimwengu wa showbiz.

Ni mwigizaji stadi, mtunzi mzuri wa mashairi, mwimbaji, produsa, na chale kwa maana kuwa anachekesha.

Vipaji vyote hivi yeye huvitumia kila anapopata fursa na matokeo yake yamekuwa ni kumwezesha kupiga hela za nguvu na pia kuwa maarufu.

MAHUSIANO