Michezo

Sylvia Kamau ateuliwa kusimamia KRU

January 17th, 2019 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Chama cha Raga kimethibitisha uteuzi wa Bi Sylvia Kamau kama Mkurugenzi Mkuu wa KRU.

Bi Kamau aliteuliwa baada ya kujiuzulu kwa Ronald Bukusi Julai 2018.

Katika taarifa, KRU ilisema, “Hatua hiyo ilikuwa muhimu hili KRU iwe na uwezo wa kushirikiana na washikadau katika ufadhili na kufanya upya operesheni zake licha ya mandhari ngumu,” lilisema shirika hilo.

Aliongoza afisi kuu ya KRU katika miradi kadhaa kama vile Safari Sevens, mashindano ya kufuzu ya Kombe la Dunia kwa wachezaji wa chini ya miaka 15 na mwanzo wa msururu wa 2018-19 HSBC World Sevens.

“Bodi inamtakia Silvia Kamau kila lema anapoanza safari hii na inawaomba washikadau wote kumuunga mkono anapoanza safari hii mpya,” ilisema.

Wakati huo, Jacob Ojee ataongoza Shujaa wakati wa mashindano Hamilton na Sydney 7 akisaidiwa na Michael Wanjala, imetangaza KRU.

Kocha mkuu Paul Murunga akizungumzia uteuzi huo alisema, “Ojee ana uwezo wa kuongoza. Tumemchunguza wakati wa mazoezi na ameonekana kuwa na uwezo wa kuhakikisha kuwa wachezaji wote wanawasiliana zaidi ya kuwa ana uzoefu katika 15s na 7s pamoja na mashindano ya kimataifa.”