Habari Mseto

Taabani kuhusu ulaghai wa mahindi

August 20th, 2020 1 min read

Na Richard Munguti

Mwanaume alishtakiwa kupokea kwa njia ya udanganyifu magunia 744 ya mahindi ya thamani ya Sh2.6m.

Peter Gachogu alishtakiwa mbele ya hakimu mkuu mahakama ya Kibera kwa ufisadi.

Bw Gachogu alikanusha shtaka hilo na kuomba aachiliwe kwa dhamana.

Kiongozi wa mashtaka hakupinga ombi hilo ila alisema kesi hiyo itaunganishwa na nyingine iltakayosikizwa hakimu Joyce Gandani Septemba 1 2020.

Mshtakiwa aliachiliwa kwa dhamana ya Sh1milioni pesa tasilimu.

Gachogu alikana kwamba kati ya Feburuari 27 na Machi 2 mwaka huu katika eneo la Viwandani Nairobi akiwa na nia ya kulaghai alipokea magunu 744 ya mahindi kutoka kwa Bi Susan Wanjiru Ngumi akidai alikuwa na uwezo ya kuyanunua.

Mahindi hayo yalikuwa na thamani ya Sh2,604,000.