Habari Mseto

Taabani kwa kuiba nyama ya Sh200,000

August 21st, 2020 1 min read

Na Richard Munguti

Muuzaji nyama alishtakiwa kuvunja na kuiba nyama na vifaa vingine vilivyo na thamani ya Sh208,600.

James Githua Maina alishtakiwa mbele ya hakimu mkuu Abdulkadir Lorot na kuiba kilo 15 za nyama za kuku na kilo 8 za nyama ya ng’ombe zenye thamani ya Sh4800.

Maina alikana kuvunja na kuiba kutoka kwa buchari ya Abdi Fatah Adinali

Wakili Sharon aliyemwakilisha mshtakiwa aliomba mshtakiwa aachiliwe kwa dhamana.

Kiongozi wa mashtaka Goerge Obiri hakupinga mshtakiwa akiachiliwa kwa dhamana.

Hakimu mkuu Abdulkadir Lorot alimwachilia kwa dhamana ya Sh200000..

Kesi itasikizwa Septemba 4