• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 8:55 AM
Atlanta yamtimua kocha Gabriel Heinze baada ya kusimamia mechi 13 pekee za MLS

Atlanta yamtimua kocha Gabriel Heinze baada ya kusimamia mechi 13 pekee za MLS

Na MASHIRIKA

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

BEKI wa zamani wa Manchester United, Gabriel Heinze, 43, amepokonywa mikoba ya ukufunzi kambini mwa Atlanta United inayoshiriki Major League Soccer (MLS) nchini Amerika na Canada.

Heinze alitimuliwa baada ya kuongoza waajiri wake kushinda mechi mbili pekee kati ya 13 alizozisimamia. Matokeo hayo yalisaza Atlanta katika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa jedwali la MLS Eastern Conference.

Rob Valentino aliyekuwa msaidizi wa Heinze sasa ameaminiwa fursa ya kushikilia mikoba ya Atlanta hadi kocha mpya atakapoajiriwa.Atlanta walioshinda taji la MLS mnamo 2018 katika msimu wao wa pili wakinogesha kipute hicho, waliongeza kwamba mbali na matokeo duni, kingine kilichochochea kutimuliwa kwa Heinze ni uhusiano mbaya kati yake na wachezaji.

Heinze ambaye pia amewahi kuchezea Real Madrid, Paris Saint-Germain (PSG) na AS Roma, aliteuliwa kuwa kocha wa Atlanta mnamo Disemba 2020 baada ya kuondoka kwa Frank de Boer aliyeaminiwa fursa ya kuwa mrithi wa Ronald Koeman katika timu ya taifa ya Uholanzi.

Hata kabla ya kubanduka Atlanta, dalili zote zilikuwa zikiashiria kwamba De Boer angepigwa kalamu kwa sababu ya matokeo duni yaliyosajiliwa na kikosi chake kwenye kipute cha MLS is Back.Heinze aliyechezea Argentina mara 72 katika enzi yake ya usogora, alisaidia Man-United kushinda taji la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo 2007 kabla ya kuhamia kambini mwa Velez Sarfield ya MLS kwa mkataba wa miaka mitatu.

Uhusiano wake na Atlanta ulianza kuingia mdudu mnamo Juni 2021 baada ya kuamuru fowadi Josef Martinez awe akijifanyia mazoezi mbali na uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo kutokana na utovu wa nidhamu.

  • Tags

You can share this post!

Al Ahly wakomoa Kaizer Cheifs na kutwaa taji la CAF...

Mvamizi kigogo Andy Carroll avunja ndoa na Newcastle United...