• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Bernardo Silva na Diogo Jota watambisha Ureno dhidi ya Azerbaijan

Bernardo Silva na Diogo Jota watambisha Ureno dhidi ya Azerbaijan

Na MASHIRIKA

USHINDI wa 3-0 uliosajiliwa na Ureno dhidi ya Azerbaijan katika mechi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za 2022 uliwapaisha miamba hao hadi kileleni mwa Kundi A mnamo Jumanne usiku.

Ureno waliotawazwa mabingwa wa bara Ulaya mnamo 2016 sasa wanajivunia alama 13, mbili zaidi kuliko nambari mbili Serbia.

Waliwekwa kifua mbele na Bernardo Silva wa Manchester City katika dakika ya 26 kabla ya kufungiwa mabao mengine ma Andre Silva na Diogo Jota aliyeshirikiana vilivyo na Bruno Fernandes.

Ushindi wa Ureno dhidi ya Azerbaijan ulisaza wenyeji wao wakivuta mkia wa Kundi A kwa alama moja. Luxembourg wanashikilia nafasi ya tatu kwa pointi sita, nne zaidi kuliko Ireland ya Kaskazini waliowalazimishia Serbia sare ya 1-1.

Ureno ambao sasa wameshinda mechi ya tatu mfululizo, walipepeta Azerbaijan bila kujivunia huduma za mshambuliaji matata Cristiano Ronaldo, aliyeonyeshwa kadi ya manjano kwa kosa la kuvua shati aliposherehekea bao katika ushindi wa awali wa 2-1 dhidi ya Ireland Kaskazini. Bao hilo la Ronaldo lilimwezesha kuvunja rekodi ya ufungaji katika ulingo wa soka ya kimataifa.

Ureno kwa sasa wamesalia na mechi tatu pekee katika safari yao ya kufuzu kuelekea Qatar mnamo 2022 na wamepangiwa kuvaana na Luxembourg mnamo Oktoba 12, 2021.

MATOKEO YA Septemba 7, 2021:

Azerbaijan 0-3 Ureno

N. Ireland 1-1 Serbia

Bosnia 2-2 Kazakhstan

Ufaransa 2-0 Finland

Austria 0-1 Scotland

Denmark 5-0 Israel

Faroes Islands 2-1 Moldova

Montenegro 0-0 Latvia

Uholanzi 6-1 Uturuki

Norway 5-1 Gibraltar

Croatia 3-0 Slovenia

Urusi 2-0 Malta

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Haaland hachoki kufunga, amepachika wavuni mabao 11...

Serikali yatahadharisha wafugaji kuhamia kaunti jirani bila...