• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 7:55 PM
‘Bobby’ Ogolla yule kipenzi cha mashabiki

‘Bobby’ Ogolla yule kipenzi cha mashabiki

Na JOHN ASHIHUNDU

USHIRIKIANO wa John Bobby Ogolla, Josephat Controller Murila, Peter Otieno Bassanga na Hussein Kheri aliacha historia katika ngome ya Harambee Stars miaka ya themanini.

Ogolla kwa jina la utani ‘The Six Million Dollar Man’ alikuwa tegemeo katika ngome hiyo ambayo jukumu lake lilikuwa kulinda kipa Mohmoud Abbas maarufu kama ‘Kenya One’.Chini ya kocha Marshall Mulwa, timu hiyo ya taifa ilitwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) mara tatu mfululizo na kuweka kombe milele.

Umakini wake katika kazi ya ukufunzi umewezesha kutoa timu nyingi kwenye ligi za chini hadi zile za juu.Mbali na Harambee Stars, Ogolla alichezea klabu ya Gor Mahia miaka ya sabini na themanini.Alibandikwa jina la The Six Million Dollar Man kutokana na ubabe wake kimaumbile.

Haikuwa rahisi kumchanganya uwanjani.Aliisaidia Gor kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati miaka ya 1980, 1081 na 1985.Alikuwa naibu wa Reinhard Fabish alipokuwa kocha wa Harambee Stars ambayo ilitinga fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika na pia alikuwa kwenye kikosi kichofika fainali ya Michezo ya Bara Afrika na kushindwa na Misri fainalini.

Mbali na Gor Mahia, Ogolla ambaye kwa sasa ndiye kocha mkuu wa Kenya Police FC pia aliwahi kufundisha Rayon Nyanza FC, Sofapaka, Gor Mahia na City Stars.Akiwa kocha wa Gor Mahia, Ogolla aliisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu, GoTV Shield na Top 8 Cup.

Kama kocha msaidizi, Ogolla alifanya kazi chini ya Len Juliens, Bobby Williams, Zdravko Lugarusic na Frank Nutal.Kocha huyo aliyezaliwa 1956 alianza kusakata soka mjini Kisumu katikati mwa miaka ya sabini kabla ya kujiunga na Gor Mahia na kuwa katika kikosi kilichotwaa ubingwa wa Kombe la Washindi barani Afrika mnamo 1987, mbali na kuisaidia klabu yake kushinda ubingwea wa ligi mara matatu- 1980, 81 na 1985.

Kadhalika alikuwa katika kikosi cha Harambee Stars kilichoshinda taji la CECAFA mara tatu mfululizo kati ya 1981 hadi 1983, kwa wakati mwingi akiibuka mlinzi bora kwenye mashindano hayo.

You can share this post!

‘Straika’ Mbrazil aliyeshindwa kupepetea K’ Ogalo

Kylian Mbappe anayeaminiwa na Paris Saint-Germain na...

T L