• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 4:36 PM
Bukayo Saka ndiye mwanasoka bora barani Ulaya miongoni mwa chipukizi 100 wasiozidi umri wa miaka 21

Bukayo Saka ndiye mwanasoka bora barani Ulaya miongoni mwa chipukizi 100 wasiozidi umri wa miaka 21

Na MASHIRIKA

BUKAYO Saka wa Arsenal ndiye mwanasoka bora barani Ulaya miongoni mwa wachezaji wenye umri usiozidi miaka 21.

Hayo ni kwa mujibu wa Shirika la CIES Football Observatory ambalo limekuwa likifuatilia ligi 32 tofauti katika mataifa ya bara Ulaya msimu huu wa 2021-22.

Miongoni mwa vigezo ambavyo vilizingatiwa na shirika hilo katika kutafuta orodha ya wanasoka 100-bora chini ya umri wa miaka 21 barani Ulaya ni uwezo wao wa kudhibiti mpira, kiwango cha kujituma ugani na uwezo wa kuelekeza mashuti yanayolenga shabaha kwenye malango ya wapinzani.

Saka, 20, amefungia Arsenal mabao 10 kutokana na mashindano yote ya hadi kufikia sasa msimu huu na anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachotegemewa na Uingereza kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar kati ya Novemba na Disemba 2022.

Jude Bellingham wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Uingereza anashikilia nafasi ya 24 kwenye orodha hiyo ya chipukizi 100-bora barani Ulaya. Kiungo huyo mvamizi mwenye umri wa miaka 18 amechezea Dortmund mara 84 tangu ajiunge nao kutoka Birmingham City mnamo 2020.

Michael Olise wa Crystal Palace anakamata nafasi ya tano huku Gabriel Martinelli wa Arsenal akiorodheshwa wa 14. Armando Broja na Valentino Livramento wa Southampton wanashikilia nafasi za 13 na 33 mtawalia. Wanasoka wengine ndani ya orodha ya 50-bora ni Rayan Ait Nouri wa Wolves, Joao Pedro wa Watford, Luke Thomas wa Leicester City na Billy Gilmour wa Norwich City.

Licha ya kutocheza mechi yoyote tangu Januari 2022 baada ya kutiwa nguvu kwa tuhuma za ubakaji nchini Uingereza, fowadi wa Manchester United, Mason Greenwood anashikilia nafasi ya pili kwenye orodha hiyo inayoongozwa na Saka.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Gonzalo Higuain kustaafu soka mwishoni mwa msimu huu wa...

Wolves wasema anayetaka kiungo wao Ruben Neves sharti aweke...

T L