• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 9:35 PM
Kadu-Asili yapata pigo kiongozi wake akihamia PAA

Kadu-Asili yapata pigo kiongozi wake akihamia PAA

NA MAUREEN ONGALA

KIONGOZI wa Kadu-Asili Gerald Thoya amekihama chama hicho na kujiunga na kile cha Pamoja African Alliance (PAA) kinachoongozwa na Gavana wa Kilifi Amason Kingi.

Bw Thoya alisema kuwa alichukua uamuzi huo baada ya kukosana na baadhi ya viongozi wa Kadu-Asili kuhusu masuala ndani ya chama huku akifichua kuwa ata – tetea kiti chake cha udiwani wadi ya Jilore kwa tiketi ya PAA.

“Kadu-Asili imekuwepo na itaendelea kuwepo ila kwa sasa ni PAA inawika na huo ndio ukweli wa mambo,” akasema Bw Thoya huku akifichua alilenga kutekeleza mageuzi ndani ya chama hicho lakini maafisa wake wakampinga.

Alitangaza kuwa amehama Kadu-Asili katika mkutano wa kisiasa kwenye kijiji cha Kakoneni, eneobunge la Malindi.

“Vyama vya kisiasa huvuma sana kutokana na yanayotekelezwa na uongozi wake. Kwa muda wa miaka miwili iliyopita nimekuwa usukani mwa Kadu-Asili na kupigania mabadiliko lakini baadhi ya viongozi

wake walikataa. Ni jambo la kusikitisha kuwa unapigania mabadiliko mazuri ila baadhi wanakataa na kutaka mambo yasalie jinsi yalivyo,” akasema Bw Thoya.

Mwanasiasa huyo alifichua kuwa alijiuzulu rasmi mnamo Februari 4 mwaka huu na sasa analenga kumakinikia kampeni zake ili kutetea kiti chake cha udiwani kupitia PAA.

Vilevile alisema kuwa licha ya kuwa na tofauti za kisiasa na Bw Kingi, yupo tayari kushirikiana na gavana huyo kuhakikisha kuwa PAA inashinda viti vingi si Kilifi pekee, bali ukanda wote wa Pwani.

“Nafikiri ni vyema kuwa tuungane pamoja. Hilo ni muhimu kwa sababu pamoja na gavana tutatambua masuala ambayo yalichangia tofauti zetu za kisiasa kisha kuyasuluhisha,” akaongeza huku akikanusha kuwa amesaliti Kadu-Asili jinsi baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakidai.

Kwa upande wake, Msemaji wa PAA Lucas Maitha alimkaribisha Bw Thoya na akafichua kuwa baa – dhi ya viongozi wa Kadu-Asili hapo awali walikataa mpango wa kuviunganisha vyama hivyo viwili kwa ajili ya umoja wa wakazi wa Pwani.

  • Tags

You can share this post!

Uhuru amtuliza Kalonzo

Jubilee yazidi kuvuna Mlimani

T L