• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 11:38 AM
Makabila makubwa yajinyakulia nafasi nyingi za ajira katika Idara ya Magereza yale madogo yakiachwa kwa mshangao

Makabila makubwa yajinyakulia nafasi nyingi za ajira katika Idara ya Magereza yale madogo yakiachwa kwa mshangao

NA CHARLES WASONGA

JAMII za Wakalenjin, Wakikuyu, Wakamba na Waluhya ndizo zilizo na uwakilishi mkubwa katika Huduma za Magereza Nchini Kenya (KPS).

Maafisa kutoka jamii hizo ndio wengi zaidi ambapo idadi ya Wakalenjin ni 5,723 wakifuatwa na Wakikuyu ambao ni 5,335 huku idadi ya maafisa kutoka jamii ya Wakamba ikiwa 3,278.

Jamii ya Waluhya inashikilia nambari nne kwa kuwakilishwa na maafisa 2,891, Waluo (maafisa 2,684) na Wakisii wanawakilishwa na jumla ya maafisa 2,536 katika huduma ya KPS.

Katika shughuli ya usajili iliyoendeshwa katika miaka ya 2019, 2020 na 2022, karibu maafisa 7,161 waliosajiliwa walitoka jamii za Wakalenjin, Wakikuyu na Wakamba.

Takwimu hizi ziliwasilishwa na Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki mnamo Alhamisi, Septemba 28, 2023, mbele ya Kamati ya Bunge kuhusu Uwiano na Usawa katika majengo ya bunge, Nairobi.

Profesa Kindiki alikuwa amealikwa na kamati hiyo kuangazia hali ya uajiri na mageuzi katika Idara ya Magereza nchini.

Waziri huyo aliungama kuwa usawa kikabila haujakuwa ukizingatiwa katika uajiri wa maafisa katika idara hiyo kwa miaka mingi.

Profesa Kindiki alitoa hakikisho kwa kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge Mwakilishi wa Kike wa Nakuru Liza Chelule, kwamba katika usajili ujao wa maafisa wa magereza usawa utadumishwa.

“Japo jamii kubwa zitapata nafasi nyingi, jamii ndogondogo pia zitatengewa nafasi zinazoendana na idadi yao,” akaeleza.

Jamii zenye uwakilishi mdogo zaidi katika Idara ya Magereza ni; Orma (maafisa 75), Rendile (62), Taveta (39), Dorobo (27, Elmolo (3), Wakenya wa asili ya Uropa (1) na Wakenya Waarabu (1).

Profesa Kindiki pia alikubali usawa haujazingatiwa katika mchakato wa kupandishwa vyeo kwa maafisa wa magereza.

“Utovu wa usawa katika upandishwaji vyeo katika Idara ya Magereza huwavunja moyo maafisa wengine ambao hutamani kupandishwa vyeo, akasema.

Profesa Kindiki alisema kuwa Wizara yake imeunda sera inayolenga kuhakikisha uwepo wa usawa wa kikabila katika uajiri na upandishwaji vyeo katika Idara ya Magereza Nchini.

  • Tags

You can share this post!

Meneja wa benki ashtakiwa kwa wizi wa Sh66.9 milioni

Demu aamua wanaommezea mate wafanye ‘interview’

T L