• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 4:36 PM
Maluda Super Cup yatinga nusu-fainali

Maluda Super Cup yatinga nusu-fainali

Na CHARLES ONGADI

KINDUMBWENDUMBWE cha Maluda Super Cup eneoubunge la Kisauni, Mombasa kimetinga hatua ya nusu fainali kwa mechi mbili kugaragazwa Jumapili na Jumatatu uwanjani Hassan Joho Girls, Utange

Timu nne; Garash Foundation, Mwavumbo United, Sokiki Youngsters na Barawa zilijipata zikiaga mashindano haya baada ya kushindwa katika hatua ya robo fainali.Sokiki Youngsters ilikuwa ya kwanza kuoneshwa mlango wa kuondokea baada ya kukwaruzwa 4-1 na Pendua Rangers katika pambano lililogaragazwa ugani Hassan Joho Girls Secondary.

Katika pambano hili , Hassan Kazungu alipachika mabao matatu kabla ya Henry Nzai kudungilia msumari wa mwisho dakika ya 78.Bao la kufutia machozi la Sokiki Youngsters likapatikana katika dakika za lala salama kupitia Abdallah Said katika dakika ya 87.

Majaoni Youngsters nao wakaibandua nje Mwavumbo United ya Mariakani, Kilifi. kwa njia ya mikwaju ya matuta (13-12) katika mchuano ulioshia sare tasa katika muda wa kawaida.Canyon Rangers inayojivunia wachezaji wengi wenye ujuzi katika mashindano sampuli hii, ikapata ushindi wa chupuchupu baada ya iliikung’uta Gharash Foundation 1-0.

Licha ya kudondoka katika pambano hili wachezaji wa Gharash Foundation walionesha mchezo wa hali ya juu kwa pasi za uhakika zilizowababatiza mno wapinzani wao.Team Control iliyo na wachezaji wa zamani wa timu ya taifa akiwemo kipa Wilson Oburu Obungu na difenda Evans Orodi ikaishinda Barawa Sportiff 3-1.

Kutokana na matokeo haya ya robo fainali, Canyon Rangers imeratibiwa kupepetana na Majaoni Youngsters siku ya Jumapili huku Pendua Rangers ikikabiliana na Team Control siku ya Jumatatu.

You can share this post!

Maandalizi ya kisasa kwa Team Kenya Jumuiya ya Madola

Gor roho mkononi ikibainika kocha Harrison hatarejea

T L