• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Masonko Saudia wamezea Ronaldo

Masonko Saudia wamezea Ronaldo

NA MASHIRIKA

MANCHESTER, UINGEREZA

SUPASTAA Cristiano Ronaldo yumo mbioni kunyakuliwa na klabu moja nchini Saudi Arabia kutoka Manchester United kwa donge nono.

Tetesi zinasema kuwa United imepokea ombi la kwanza kutoka kwa klabu hiyo inayotaka huduma za mshambulizi huyo Mreno anayesemekana atatia kibindoni Sh14.7 bilioni kila mwaka akikubali ofa hiyo.

Mshindi huyo mara tano wa tuzo ya mwanasoka bora duniani anaaminika anatamani kuondoka Old Trafford kutafuta kibarua kitakachopima uwezo wake zaidi baada ya kusikitishwa na United kukosa kufuzu kwa Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao.

Miamba Bayern Munich, Chelsea na Napoli wanaaminika kuvutiwa na Ronaldo, lakini hakuna kati yao aliyeweka ofa yoyote mezani.

Gumzo sasa linafichua kuwa klabu moja nchini Saudia, ambayo bado haijatajwa, imetokea ikiwa ya kwanza kuomba huduma zake katika mpango utakaompa Ronaldo mshahara unaozidi Sh14.0 bilioni kila msimu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la CNN nchini Ureno, ofa inajumuisha ada ya uhamisho ya karibu Sh4.2 bilioni, ambayo inapita Sh1.7 bilioni ambazo United ilitumia kumnyakua kutoka Juventus mwaka jana.

Ronaldo, kisha, atapokea jumla ya Sh29.4 bilioni katika kandarasi ya miaka miwili, huku kiasi kingine cha Sh2.8 bilioni kikiwa ni ada ya ajenti.

Ronaldo alipewa ruhusa maalum kuchelewa kurejea United kwa sababu za kifamilia na bado hajafahamisha viongozi wa klabu hiyo atarejea lini Manchester kwa msimu mpya.

Anasemekana kukerwa na matokeo ya United yaliyoikosesha fura bomba ya kushiriki Klabu Bingwa Ulaya baada ya kumaliza Ligi Kuu (EPL) katika nafasi ya sita na pia kutotetemesha sokoni katika kipindi kirefu cha uhamisho.

Dili hii ikifaulu, fumbwe huyo atatia mfukoni tita la Sh28 bilioni kila mwaka kwa miaka miwili kama mshahara; chambo kinachoweza kumbandua Manchester United

  • Tags

You can share this post!

Amerika kupunguza mapato ya mafuta yanayotoka Urusi

Ufisadi: Karua atia ahadi yake doa kuu

T L