• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 9:35 PM
Mzozo wa mpaka eneo la Maseno walipuka upya

Mzozo wa mpaka eneo la Maseno walipuka upya

Na BENSON AMADALA

MZOZO kuhusu mpaka katika Vihiga na Kisumu eneo la Maseno umezuka upya viongozi wa kaunti zote mbili wakitaka serikali iingilie kati.

Haya yalitokea siku chache baada ya mkutano wa Kiuchumi wa kaunti za kanda ya Ziwa Victoria uliofanyika Kaunti ya Kakamega. Gavana wa Vihiga, Wilber Ottichilo alilalamika kuwa bunge la Kitaifa na kamati ya seneti zilichelewa kusuluhisha mgogoro huo.

“Kamati ya seneti na bunge la Kitaifa ziliingilia suala hili. Hata hivyo hatujapata suluhu yoyote,” akasema Bw Ottichilo. Hata hivyo, Gavana wa Kisumu, Profesa Anyang’ Nyong’o alikasirishwa na matamshi hayo ya Bw Ottichilo huku akidai kuwa serikali yake itashikilia msimamo wake kuhusu suala hilo.

Kaunti hizo mbili zinadai zinamiliki Maseno.

You can share this post!

Polisi aua 7 akiwemo mkewe kabla kujiua

Fahamu mengi kuhusu nyama ya sungura

T L