• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 5:22 PM
Shabiki Isaac Juma azikwa kishujaa Kakamega

Shabiki Isaac Juma azikwa kishujaa Kakamega

Na JOHN ASHIHUNDU

Itachukuwa muda mrefu Wakenya kusahau hafla ya kumuaga shabiki shujaa wa kandanda Isaac Juma aliyezikwa wikendi iliyopita katika kijiji cha Ebuyenjele, Mumias Mashariki, Kaunti ya Kakamega.

Ni tukio ambao halitasahulika kutokana na jinsi lilivyovutia watu maarufu na majagina wa michezo, pamoja na wanasiasa wa viwango tofauti wakiongozwa na Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya. Mashabiki wa tabala mbali mbali walijitolea siku huyo, huku wakiwa wamejipaka rangi za kila aina kumpa buriani mwenzao ambaye aliuawa kinyama wiki tatu zilizopita.

Kwa wale ambao hawakupata nafasi ya kuhudhuria mazisho hayo, kwa hakika ya Juma yalifanyika kwa njia ya kipekee. Shabiki huyo wa klabu ya AFC Leopards pamoja na timu ya taifa Harambee Stars alipewa heshima ambazo  hazijawahi kupewa shabiki mwingine yeyote aliyeaga nchini Kenya.

Eneo hafla hiyo ilifanyika zilipambwa kwa bendera ya kitaifa wakati wa hafla hiyo iliyoendeshwa na mashabiki wenzake sugu wakiongozwa na Jaro Soja ambaye ni shabiki mkuu wa klabu ya Gor Mahia FC. Juma ambaye pia alijulikana kama Ingwe alivamiwa nyumbani kwake na watu waliokuwa na silaha ambao walimkatakata kwa panga, huku mtoto wake akinusurika mwenye umri wa miaka 18 akinusurika kifo.

Tayari watu wawili wamesanswa kwa kuhusishwa na kifo chake kilichotokana na mzozo wa ardhi. Mashabiki sugu kutoka mataifa ya kigeni kama Uganda na Tanzania ni miongoni mwa waliohudhuria mazishi ya shabiki huyo aliefariki akiwa na umria wa miaka 55.

Jaro Soja (kushoto) miongoni mwa mashabiki walihudhuria mazishi ya Juma. Kulia ni mwenyeiti wa Chama cha Mashabiki wa Soka Kenya (Kefafa), Francis Liboyi…Picha/JOHN ASHIHUNDU

Mbali na kuhudhuriwa na watu wa hadhi ya juu, kadhalika matangaza ya shabiki huyo yatakumbukwa kuwa miongoni mwa yale ya bei ghali. Kawaida, gharama ya matanga kwa mtu wa kawaida kiwango cha Juma ni karibu Sh300,000, lakini Juma yaligharimu zaidi ya Sh1 milioni, mbali na jeneza lilogharimu zaidi ya Sh40,000.

N’gombe kadhaa walichinjwa na kupikiwa waombolezaji. Kadhalika kulikuwa na vinywaji kwa wageni waliofika kwenye hafla hiyo ya kukata na shoka. Wasanii wa kila aina wakiwemo Ineah Mukaisi na Ken Khwesa “Shitsulenje” pia walihudhuria kwa lengo la kutumbuiza wageni waliofika siku hiyo.

Kwa jumla, mazishia ya Juma yalihudhuriwa na zaidi ya watu 5,000, baadhi yao wakiwa wamevalia mavazi ya timu wanazounga mkono. Hafla ilianza kwa safari ya kutoka chumba cha kuhifadhi mati cha Butere ambao mwili ulipelekwa Mumias Sports Complex kwa umma kupata fursa ya kuutazama.

Baadaye msafara wa magari yaliyombeba yakizunguka mjini Mumias kabla ya kuelekea bomani. Shabiki Jaro Soja ni miongoni mwalioeleza jinsi Juma alivyosafiri naye katika mataifa ya kigeni kushangilia Harambee Stars. Kadhalika alieleza jinsi Juma alivyodhoofika kila wakati timu yake ilivyocheza vibaya.

Mbali na sherehe za mila na tamaduni za Wanga, misa ya ufu iliongozwa na padre Gabriel Oduori wa Mtakatifu Beda. Miongoni mwa wanasiasa waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na wabunge, madiwani na Fernandez Barasa anayewania kiti cha kuwa Gavana wa Kakamega.

Juma alifahamika kutokana na ushabiki wake wa kipekee, ukiwemo kukimbia uwanjani na kupingirika kila wakati timu yake ilipofunga bao. Kutokana na ushabiki wake, kampuni ya Betika imetangaza kuichengea familia yake nyumba ya kifarahi mara tu watakapohama eneo walikomzika Juma.

Serikali ya Kaunti ya Kakamega imeahidi kulipa karo ya watoto wake watatu walio sekondari, huku Barasa aliahidi kugahramia karo yaw engine wakaofanya mtihati wa darasa la nane mwaka huu. Kupitia kwa Chris Onguso, Betika ilipeana Sh500,000 kwa familia ya marehemu, huku Mbunge wa Mumias Mashariki Johnston Naicca akipeana Sh100,000.

Gavana Oparanya alichangisha zaidi ya Sh350,000 kusaidia familia ya Juma ambaye ameacha wajane wawili Christine na Faridah. Michango zaidi ya pesa ilitoka kwa matawi ya klabu ya AFC Leopards pamoja na klabu nyingi za ligi kuu zikiongozwa na mabingwa watetezi Gor Mahia.

Juma atakumbukwa kama shabiki nambari moja aliyejitolea kutumbuiza uwanjani wakati mechi zikiendelea. Mbali na kandanda, kadhalika Juma alikuwa shabiki mkubwa wa mpira wa raga, voliboli na mashindano ya riadha. Atakumbukwa milele kutokana na msaada wake mkubwa katika kufanikisha na kuinua soka nchini kwa jumla.

Kutokana na umaarufu wake, risala za rambi rambi zilitumwa na watu maarufu akiwemo mwanasiasa maarufu na kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga aliyemfahamu kama rafikye wa karibu. Mlezi wa AFC Leopards, Musalia Mudavadi pamoja na Naibu wa Rais William Ruto pia walituma risala zao.

Chama cha Mashabiki wa Soka Nchini (Kefofa) kupitia kwa mwenyekiti wake, Francis Liboyi kilitaja kifoa chake kama pigo kubwa kwa muungano wao, huku kikisema kitaendelea kumkumbuka kutokana na jinsi alivyoshabiki timu za taifa. Juma ambaye ni miongoni mwa mashabiki wachache waklioufanya mchezo kuvutia zaidi, ameacha watoto 17.

Mashabiki wawili wa Gor Mahia wakisimama wima kwenye mavazi yao ya kijani…Picha/JOHN ASHIHUNDU

 

You can share this post!

UDA yatangaza tarehe za mchujo

Maseneta wagonga mwamba

T L