NA KNA
MBUNGE maalum ambaye pia ni mwaniaji wa kiti cha useneta Kaunti ya Bomet, Bw Wilson Sossion (pichani), ameingia katika maeleweno na wafanyabiashara wa kaunti hiyo kuunda kamati za usimamizi katika kaunti ndogo.
Akizungumza katika ofisi za Chama cha Wafanyabiashara mjini Bomet, alisema utafiti waonyesha kuwa kaunti hiyo ina viwango vya juu vya umasikini huku ukusanyaji wa mapato ukiwa duni.