• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 5:07 PM
TUSIJE TUKASAHAU

TUSIJE TUKASAHAU

SERIKALI kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Ujasirimali imekuwa ikiendeleza sera ya “Nunua Kenya, Jenga Kenya” ili kufanikisha mojawapo ya nguzo za Ajenda Nne Kuu za Maendeleo – utengenezaji bidhaa.

Lakini Waziri Betty Maina anayesimamia wizara hiyo asisahau kwamba Wakenya wanamsubiri kwa hamu na ghamu kutekeleza ufufuzi wa kampuni za kutengeneza nguo za Kisumu Cotton Mills (Kicomi) na Mount Kenya Textile (Mountex), alivyoahidi Rais Uhuru Kenyatta.

Kiongozi wa taifa alitoa ahadi hiyo mnamo Juni 22, 2019 alipoongoza hafla ya ufunguzi rasmi wa kiwanda cha kutengeneza nguo cha Rivatex, Eldoret, kilichofanyiwa ukarabati kwa gharama ya Sh5 bilioni.

Ahadi

Huku Wizara ya Bi Maina ikiendelea kuwahimiza Wakenya kununua na kuvaa nguo zilizotengenezwa humu nchini badala ya zile za mitumba zilizoagizwa kutoka ng’ambo isihahau kufanikisha ndoto ya ufufuzi wa viwanda hivi.

You can share this post!

Jinsi ya kutunza vidole na kucha

Kinoti awaambia wabunge kwamba mwili wa Agnes Wanjiru...

T L