TAHARIRI: Twapongeza wanariadha wetu kuletea Kenya fahari

TAHARIRI: Twapongeza wanariadha wetu kuletea Kenya fahari

NA MHARIRI

NI heshima ya kipekee kwa kila Mkenya kushuhudia mwenzao akisifiwa na kutambuliwa kote duniani kwa kuwa bora zaidi katika fani fulani ya spoti huku ulimwengu mzima ukitazama.

Kutoka pembe zote za dunia, wanariadha wa Kenya walishangaza kwa kufana katika mbio mbalimbali kwa kunyakua medali kadhaa zikiwepo za dhahabu, fedha na shaba kwenye mashinadano yanayoendelea mjini Cali, Colombia na Birmingham, Uingereza.

Michezo inayoendelea Colombia ni ya vijana wa umri wa chini ya miaka 20 huku ile ya Uingereza ikiwa ya watu wazima. Kufikia sasa tayari Kenya ina medali sita za vijana na nane za wazima.

Wakimbiaji wetu walidhihirisha ushujaa wao kwa kupigana kwa uwezo wao wote kuhakikisha wameweka taifa lao mbele katika ramani ya kimataifa.

Kwa wale walioshinda au kushindwa bila shaka kwa maantiki hii ni mashujaa kwa vile walivyowakilisha nchi yao ifaavyo na kwa kujitolea.Wakenya waliwatambua kwa njia ya kipekee walioshindia taifa angalau medali hasa kupitia jumbe zao za pongezi kwenye mitandao tofauti tofauti ya kijamii.

Mmoja kati ya walioteka hisia za raia wengi ni Ferdinand Omanyala aliyeshindia Kenya dhahabu ya kwanza katika mita 100 kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Birmingham, Uingereza.

Wengine waliofanya vyema ni Daniel Simiu katika mbio za 10,000m wanaume, Irene Cheptai 10, 000 wanawake na Margaret Wangari katika marathon. Wote hawa walishinda nishani za fedha.

Mashujaa wengine ni washindi wa medali ya shaba ambao ni Kibiwott Kandie katika 10. 000m, Michael Githae kwenye marathon na Hellen Wawira ambaye ni mnyanyuaji uzito.

Barobaro wa Kenya walitamalaki zaidi kwa kushinda dhahabu tatu wakijumuisha Reynold Cheruiyot (1,500m), Betty Chelangat (3,000m) na Faith Cherotich (3,000m kuruka viunzi na maji).

Damaris Mutunga alitwaa fedha katika 400m huku wenzake Daniel Kimaiyo na Nancy Cherop wakinyakua shaba katika mbio za 1,500m na 3,000m mtawalia.

Ni funzo la moja kwa moja kutoka kwa wachezaji wetu kwamba, kila Mkenya awaye yoyote afaa kuwa tayari kuipigania hadi kufa taifa lake. Uzalendo unafaa kuanzia kwa viongozi na wanaoongozwa yaani watawala na wataliwa.

Hivyo basi, uchaguzi unapokaribia ni vyema wanaochaguana wawateue watu wanaoweza kuaminika kuwa mashujaa kwani wakifanya hivi nao watakuwa wamedhihirisha ushujaa wao.

kikamilifu. Kuzingatia amani wakati wa kura ni njia nyingine na kudhirika mapenzi hakika nchi yetu.

You can share this post!

Sadio Mane aongoza Bayern kubomoa Frankfurt katika...

Soko China: Kilimo cha avokado kunoga nchini Kenya

T L