• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 11:38 AM
Ada mpya ya NSSF yapingwa mahakamani

Ada mpya ya NSSF yapingwa mahakamani

NA RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA Kuu imeombwa ifutilie mbali ada mpya ya malipo ya uzeeni (NSSF) iliyopitishwa hivi majuzi.

Wakili John Maina Ndegwa anayeomba mahakama iratibishe kesi hiyo kuwa ya dharura, amedokeza kuwa ada hiyo mpya inalenga kufilisisha kampuni, hali anayodai itasababisha idadi kubwa ya watu kutimuliwa kazini.

Ada hiyo mpya itaanza kutekelezwa Februari 2024.

Bw Ndegwa amedokeza kuwa kutekelezwa kwa ada hii mpya ya NSSF kutaathiri pakubwa uchumi wa taifa hili.

“Kutekelezwa kwa ada hii mpya kutasababisha waajiri wengi kuchukua hatua ya kuwaachisha kazi maelfu ya wafanyakazi,” akadokeza Bw Ndegwa.

Wakili huyo alisema kuwa ada hii mpya imepitishwa wakati nchi hii inakumbwa na gharama ya juu ya maisha huku wafanyakazi wakilemewa na mzigo wa kodi nyingi wanazolazimika kulipa.

Anaiomba Mahakama Kuu iratibishe kesi hiyo kuwa ya dharura na kuzima hatua ya bodi ya NSSF kutekeleza nyongeza hiyo mpya ya 2024.

“Sheria ya NSSF kifungu cha 3 iliyopitishwa 2013 imeweka bayana pesa anazofaa kukatwa kila mfanyakazi kwa muda wa miaka minne kuanzia Januari 2014,” akasema Bw Ndegwa.

Ada hiyo mpya inalingana na mishahara. Wafanyakazi wanaopata mshahara wa chini wanapaswa kuwa wale wanaopokea Sh7,000. Mshahara huu ulipandishwa kutoka Sh6,000. Kwa wale wanaopokea mshahara huu, mmoja anatakiwa kulipa ada mpya ya Sh420 kutoka Sh360.

Wale wanaopokea mshahara wa juu ni wale wanaopokea Sh29,000. Wafanyakazi hawa wametengewa kiwango cha Sh1,740 badala ya Sh1,080 walizokuwa wanalipa hapo awali.

Kile mfanyakazi kazi anacholipa pia mwajiri ataongeza kiwango sawa na hicho.

Ada hii mpya itatathiminiwa upya Januari 2025.

  • Tags

You can share this post!

Spika Mwambire asisitiza Mung’aro hajageuza bunge la...

Mudavadi aongezewa majukumu serikalini, Gachagua akilumbana...

T L