• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 5:55 AM
Garissa, Kwale zilikuwa na watahiniwa wengi walio na umri mkubwa

Garissa, Kwale zilikuwa na watahiniwa wengi walio na umri mkubwa

Na BENSON MATHEKA

Kaunti sita zilikuwa na watahiniwa wa umri wa miaka 18 na zaidi katika mtihani wa KCPE wa mwaka huu.

Akitangaza matokeo ya mwaka huu ya mtihani huo, Waziri wa Elimu, Ezekiel Machogu alitaja kaunti hizo kama Garissa ambayo asilimia 25.86 ya waliofanya mtihani huo walikuwa watu wazima, Turkana (asilimia 24.5), Kwale (asilimia 16.09), Kilifi (asilimia 15.66) na Mandera ( asilimia 33.90).

Wakati huo huo, kaunti tano za Baringo, Wajir, Bomet, Kericho na Pokot Magharibi zilikuwa na idadi kubwa ya watahiniwa katika KCPE waliokuwa na umri wa chini ya miaka 12.

Bw Machogu alisema kwamba, idadi kubwa ya watahiniwa katika KCPE ya mwaka huu walikuwa na umri wa kati ya miaka 13 na 15 wakiwa ni 1,023,859.( asilimia 72.31) ya watahiniwa wote.

Alisema kwamba, ingawa KCPE ilisaidia kuafikia usawa wa jinsia katika elimu, ni kaunti ya Isiolo pekee iliyoongoza kwa kuwa na watahiniwa wengi wasichana kuliko wavulana.

Kaunti kumi za Mandera, Garissa, Turkana, Wajir, Machakos, Nyamira, Samburu Baringo, Nandi na Makueni zilikuwa na pengo kubwa kati ya wavulana na wasichana waliofanya KCPE mwaka huu.

  • Tags

You can share this post!

Chunga usiwe ‘mzazi hewa’ kwenye maisha ya mwanao

Kalameni akemea ex wake kwa kumwandama warudiane

T L