• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 8:27 PM
Ghana kukita kambi Naivasha kujiandaa kupiga Ethiopia

Ghana kukita kambi Naivasha kujiandaa kupiga Ethiopia

Na GEOFFREY ANENE

TIMU ya taifa ya soka ya Ghana almaarufu Black Stars inatarajiwa kuanza kuwasili nchini Kenya mnamo Novemba 12 kujiandaa kwa mechi ya kufuzu kushiriki Kombe la Afrika (AFCON) mwaka 2019 dhidi ya Ethiopia itakayosakatwa Novemba 18, 2018 jijini Addis Ababa.

Vyombo vya habari nchini Ghana vimeripoti Jumatatu kwamba wachezaji wote 20 waliitiwa na kocha Kwesi Appiah wanatarajiwa kukusanyika mjini Naivasha kwa vipindi vitano vya mazoezi kabla ya kuelekea Ethiopia kuvaana na Walias.

Ghana inashikilia nafasi ya tatu kwa alama tatu nyuma ya viongozi Kenya, ambao wamezoa alama saba, na nambari mbili Ethiopia, ambao wamevuna alama nne.

Vijana wa Appiah wanahitaji kushinda Ethiopia ili kuimarisha nafasi ya kushiriki AFCON nchini Cameroon mwaka 2019.

Baada ya kuwaacha wachezaji matata Asamoah Gyan na ndugu Andre Ayew na Jordan Ayew kwa mechi dhidi ya Kenya mwezi Oktoba, Appiah amewarudisha kikosini kwa mchuano huu muhimu.

Kikosi cha Ghana: Wachezaji – Richard Ofori (Martizburg, Afrika Kusini), Lawrence Ati (Sochaux, Ufaransa), Harrison Afful (Columbus Crew, Marekani), John Boye (Metz, Ufaransa), Lumor Agbenyenu (Sporting, Ureno), Andy Yiadom (Reading, Uingereza), Jonathan Mensah (Columbus Crew, Marekani), Kassim Nuhu (Hoffenheim, Ujerumani), Andre Ayew (Fenerbahce, Uturuki), Mubarak Wakaso (Alaves, Uhispania), Kwadwo Asamoah (Inter Milan, Italia), Afriyie Acquah (Empoli, Italia), Christian Atsu (Newcastle, Uingereza), Nana Ampomah (Waasland-Beveren, Ubelgiji), Thomas Partey (Atletico Madrid, Uhispania), Majeed Ashimeru (St Gallen, Uswizi), Jordan Ayew (Crystal Palace, Uingereza), Asamoah Gyan (Kayserispor, Uturuki), Majeed Waris (Nantes, Ufaransa) na Emmanuel Boateng (Levante, Uhispania).

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Serikali isiwatie hofu watahiniwa

Messi kupoteza mkewe asipomkoma Miss BumBum

adminleo