• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 9:12 AM
Isaac Mwaura ateuliwa Msemaji wa Serikali

Isaac Mwaura ateuliwa Msemaji wa Serikali

NA SAMMY WAWERU

ALIYEKUWA Waziri Msaidizi (CAS) mteule katika Afisi ya Mkuu wa Mawaziri, Isaac Mwaura ameteuliwa kama Msemaji wa Serikali ya Kenya Kwanza.

Bw Mwaura, ambaye amewahi kuhudumu kama Seneta Maalum, amepata wadhifa huo kufuatia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyotangazwa na Rais William Ruto Jumatano, Oktoba 4, 2023 kupitia notisi iliyotolewa na Mkuu wa Utumishi wa Umma, Felix Koskei.

Atasaidiwa na manaibu; Mwanaisha Chidzuga na Gabriel Muthuma.

Mwanahabari Mwanaisha Chidzuga ambaye aligombea kiti cha Matuga Kaunti ya Kwale katika uchaguzi mkuu wa 2022 lakini akapoteza. Ameteuliwa Naibu Msemaji wa Serikali. Picha|Maktaba

Bw Hussein Mohamed, mtangazaji wa zamani, ndiye alikuwa akitoa taarifa za serikali licha ya kuwa Msemaji wa Ikulu.

“Kufuatia pendekezo la Utumishi wa Umma, Afisi ya Msemaji wa Serikali imefanyiwa mabadiliko na Mheshimiwa Isaac Maigua Mwaura ameteuliwa kuingoza, manaibu wake wakiwa Mwanaisha Chidzuga na Gabriel Muthuma,” notisi iliyotiwa saini na Bw Koskei inaeleza.

Mwaka uliopita, Bw Mwaura alimenyana na mbunge wa sasa Ruiru Simon King’ara kupata tikiti ya chama cha UDA kuwania kiti hicho cha kisiasa.

Mwaura pia amewahi kuhudumu kama Seneta Maalum chini ya chama cha upinzani cha ODM.

  • Tags

You can share this post!

Mudavadi apokonya Mutua wizara ya Mashauri ya Kigeni kwenye...

Pasta amenitunga mimba kisha akaniruka!

T L