• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 11:38 AM
Kafyu Baringo, Pokot Magharibi na Elgeyo Marakwet haitasitishwa – serikali yashikilia

Kafyu Baringo, Pokot Magharibi na Elgeyo Marakwet haitasitishwa – serikali yashikilia

FLORAH KOECH Na CHARLES WASONGA

SERIKALI imeshikilia kuwa kafyu iliyowekwa katika kaunti tatu zilizokumbwa na mapigano kaskazini mwa bonde la ufa haitaondolewa hadi usalama urejee maeneo hayo.

Kamishna wa Ukanda wa Bonde la Ufa Maalim Mohamed alisema kuwa visa vya wizi wa mifugo vingali vinashuhudiwa katika kaunti za Baringo, Elgeyo Marakwet na Pokot Magharibi hata baada ya serikali kutangaza kafyu kuanzia Juni 7.

“Kafyu itaendelea kwa sababu wakazi wamedinda kutia amri inayowataka kusalimisha silaha haramu. Wamekataa kutoa nafasi kwa mazungumzo na ndio maana tunaendelea kushuhudia vita,” akasema Bw Mohamed.

  • Tags

You can share this post!

‘Jicho la Jahazi’ lilivyogeuka kuwa kitambulisho cha...

Kampuni yazindua vitafunio vilivyosindikwa kwa nyama ya kuku

T L