• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 6:50 PM
Kibicho aendeleza siasa, akanusha kutumia mabavu dhidi ya UDA

Kibicho aendeleza siasa, akanusha kutumia mabavu dhidi ya UDA

NA GEORGE MUNENE

KATIBU katika Wizara ya Usalama, Karanja Kibicho amekana madai kuwa anawatisha wawaniaji wa viti mbalimbali kwa tiketi ya chama cha United Democratic Alliance (UDA) kusudi wajiunge na Jubilee.

“Hawa wanasiasa wananigeukia baada ya kugundua kuwa mawimbi ya kisiasa ya UDA yamefifia, ishara kwamba watapoteza katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9,” Dkt Kibicho akasema Jumamosi mjini Kagio, Kaunti ya Kirinyaga.

Alitoa kauli hiyo baada ya kuwapokea wanachama 50 wa UDA waliohamia chama cha Jubilee.

Dkt Kibicho pia aliwakashifu wandani wa Naibu Rais William Ruto akisema wamebuni mwenendo wa kutaja jina lake wanaposhindwa kufikia malengo yao ya kisiasa.

“Hakuna mtu anayelazimishwa kujiunga na Jubilee. Sijatoa vitisho kwa mtu yeyote kumlazimisha kutoka kule kuja huku,” akaeleza.

Katika siku za majuzi baadhi ya wanasiasa eneo la Mlima Kenya wamekuwa wakihama UDA na kujiunga tena na Jubilee. wakijipanga kuwania viti mbalimbali katika uchaguzi mkuu ujao.

“Ni haki ya Wakenya kuhamia chama chochote kile kwa sababu hiyo ni haki yao ya kikatiba,” Dkt Kibicho akasema, akiapa kuendeleza kile alichokitaja kama, ‘elimu ya uraia”.

  • Tags

You can share this post!

Polisi wapeleleza kifo cha kijana katika kampeni za Malala...

TUSIJE TUKASAHAU: Munya asije akasahau Kiunjuri aliwezesha...

T L