• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
LSK kuchunguza kiini cha nusu ya wanasheria kufeli mtihani

LSK kuchunguza kiini cha nusu ya wanasheria kufeli mtihani

Na ERIC MATARA

Chama cha Wanasheria nchini (LSK), kimeanza kuchunguza sababu za wanafunzi wanaofanya mithani wa kuhitimu uanasheria katika chuo cha mafunzo ya taaluma hiyo nchini (KSL), kufeli kwa wingi.

Katika miaka minane iliyopita, wanafunzi wanaofanya mtihani huo wamekuwa wakifeli kwa wingi, jambo ambalo limetia wadau wasiwasi.

Afisa Mkuu Mtendaji wa LSK, Mercy Wambua, alisema kwamba chama hicho kimeunda kamati ya kuchunguza sababu zinazofanya wanafunzi wengi wanaofanya mtihani huo kufeli.

“LSK imeunda kamati ya kuchunguza kufeli kwa wanafunzi wanaopata mafunzo ya uanasheria. Hii ni kufuatia uamuzi uliotolewa na Jaji John Mativo ambaye aliagiza uchunguzi kuhusu idadi kubwa ya mawakili wanaokosa kufaulu wakifanya mtihani huo,” alisema Bi Wambua.

Jaji Mativo aliagiza LSK ikabidhiwe uamuzi huo ili kufanya uchunguzi kubaini sababu ya wanaofanya mtihani huo katika KSL kutofaulu.

Bi Wambua alisema kamati inayosimamiwa na wakili Esther Chege tayari imeanza kazi yake na itatoa ripoti yake hivi karibuni.

Kamati hiyo pia itachunguza masuala mengine yanayoathiri mafunzo ya mawakili ikiwa ni pamoja na kubaini ikiwa yanawiana na viwango vya kimataifa, gharama ya mafunzo na mtaala wa sasa.

Aidha, kamati itahusisha wadau wengine ikiwa ni pamoja na vyuo vikuu, Tume ya Elimu ya Juu na Baraza la Masomo ya Uanasheria.

You can share this post!

Ugomvi wa penzi wazua mauti ya mtoto

Wandani wa Ruto waapa kuupinga mswada wa jinsia

adminleo