• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:33 AM
Madoli ya ngono kuharibiwa na KRA

Madoli ya ngono kuharibiwa na KRA

NA CHARLES WASONGA

MADOLI yanayotumika na wanaume kujiridhisha kimapenzi (sex toys) na uume bandia (artificial male organs) ni miongoni mwa bidhaa zilizoagizwa nje ambazo zitaharibiwa na Mamlaka ya Ushuru Nchini (KRA) baada ya kukosa kuchukuliwa na wenyewe kutoka mabohari yake kadhaa eneo la Rift Valley.

Hii ni baada ya kukamilika kwa muda makataa ya siku 30 ambayo KRA ilitoa kwa wenye bidhaa hizo kuzichukua kutoka mabohari yake ya Eldoret, Nakuru, Lodwar, Lokichoggio na Suam.

Bidhaa hizo sasa zitaharibiwa mnamo Jumatatu, Mei, 22, 2023 baada ya muda KRA kutoa notisi kwa wenyewe kuzichukua mnamo Aprili 20, 2023.

“Notisi inatolewa kwamba ikiwa bidhaa zilizotajwa hapa chini hazitaondolewa katika mabohari ndani ya siku 30 baada ya kutolewa kwa notisi, zitachukuliwa kama bidhaa zilizotelekezwa na zitaharibiwa kulingana maagizo ya Kamishna Mei 22, 2022,” ikasema notisi iliyochapishwa katika gazeti rasmi la serikali.

Bidhaa nyingine ambazo zitaharibiwa ni pombe, balbu, blanketi na mbegu zilizoko katika bohari la Eldoret.

Bidhaa nyingine zitakazotupwa ni mamia ya magunia ya sukari, kreti kadha za pombe za bia na maziwa ya unga katika bohari la KRA mjini Lodwar, katika Kaunti ya Turkana.

Mali nyingine iliyoko kwenye bohari hilo na itakayoharibiwa ni pamoja na katoni 100 za sigara aina ya Supermatch, gari moja aina ya Toyota Hilux, gari aina ya Mitsubishi Colt na aina mbalimbali za mitambo ya mawasiliano.

Aidha, chupi, magwanda ya kijeshi, dawa za kuangamiza wadudu na bunduki bandia zilizoko katika bohari la Nakuru pia zitaharibiwa mnamo Mei 22, 2023.

Magunia 26 ya sukari yaliyoko katika ghala la Suam, pia yataharibiwa.

  • Tags

You can share this post!

NDC ya Jubilee kufanyika licha ya ‘vijimambo’

Nilitamani Raila ashinde urais mwaka 2013 – Issack...

T L