• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 6:55 PM
Masomo yasitishwa Shule ya Upili ya Bahati, Nakuru

Masomo yasitishwa Shule ya Upili ya Bahati, Nakuru

NA FAUSTINE NGILA

Shughuli za masomo kwenye Shule ya Upili ya Bahati Kaunti ya Nakuru zilisitishwa Alhamisi asubuhi baada ya wanafunzi 68 na walimu watano kupatikana na virusi vya corona.

Afisa wa Afya wa Kaunti hiyo Kariuki Gichuki alithibitisha hayo kwamba mwanafunzi mmoja alikuwa amekimbizwa hospitali ya Nakuru na kulazwa maeneo ya kutengwa baada ya kupata matatizo ya kupumua.

“Hiki ni kisa cha kusikitisha lakini maafisa wa afya wametumwa shuleni humo ili kuangalia hali ya walimu na wanafunzi waliokotengwa pamoja na wanafunzi,”alisema Dkt Gichuki.

Alisema kwamba wanafunzi 115 waliwekwa kwenye karantini  shuleni na sampuli nyingi zinaendela kuchukuliwa ili kupimwa.

Kulingana na Dkt Gichuki shule zimekuwa maeneo yanayoathirika san ana vieusi vya corona hivi karibuni lakini akasema kwamba tmu spesheli lilikuwa limetumwa ili kuchunguza na kuzuia maambukizi kwenye vyuo na shule Kaunti hiyo.

“Programu hiyo inawalenga wanafunzi na walimu pamoja na wafanyakzi wa shule,” alisema.

Mkuu wa maswala ya afya ya jamii Samuel King’ori alisema kwamba kvalia barakoa kutababiki jambo la lazima hadi pale mamabukizi ya corona yatakapo isha.Aliogoza kwa kutotilia maanani maagizo ya wizara ya afya imekuwa chanzo kubwa cha maambukizi.

“Ni onyyo kwa wale ambao hawavalii maski kwamba watakamatwa na kushtakiwa,”alisema Bw King’ori.

  • Tags

You can share this post!

Polisi wamsaka mwalimu aliyotoroka karantini

Bunge kuzindua kanuni zake katika Kiswahili leo